Searching...
Image and video hosting by TinyPic
15 April 2014
Tuesday, April 15, 2014

STEVEN GERRARD:NAJIHISI KAMA NINA MIAKA 21 TENA.



Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Steven Gerrard ameweka wazi umuhimu ambao utawapa ushindi wa Ligi ya Premia baada ya kucheza soka la kulipwa miaka 17 kwa kutangaza kuwa mwezi ujao utakuwa ‘mkuu zaidi’ katika uchezaji wake. 

Kwenye uchezaji wake ambapo amechezea klabu moja pekee, nahodha wa Gerrard amejishindia Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, Kombe la Uefa na Vikombe viwili vya League na ameichezea Uingereza mechi 109, lakini ushindi wa ligi umempiga chenga. 

Kiungo huyo wa kati wa miaka 33 alitawazwa mchezaji bora wa mechi, hata hivyo, huku Liverpool wakijipatia udhibiti wa safari ya kujishindia taji la kwanza la Uingereza tangu 1990 kwa ushindi wa kusisimua wa 3-2 dhidi ya Manchester City katika uwanja uliojaa hisia wa Anfield Jumapili.

Gerrard alisema uchezaji huo ulikuwa “ujumbe mkuu zaidi” ambao Liverpool imetoa kwenye kampeni ya sasa lakini akakiri kwamba “alihofia mabaya” City walipotoka nyuma 2-0 na kusawazisha 2-2 kabla ya bao la ushindi la dakika za mwisho kutoka kwa Philippe Coutinho. 

“Ninafikiri huo ndio uchezaji bora zaidi wetu msimu wote,” aliambia runinga ya klabu hiyo.
“Kwa dakika za kwanza 30-35, nilifikiri tuliwaelemea kabisa timu ambayo imechukuliwa kuwa bora zaidi kwenye ligi. Na hata tungepata mabao matatu au manne. 

“Lakini hiyo ni timu kuu, wana wachezaji nyota, wana wachezaji wa thamani ya pauni 30-40 milioni wanaotoka benchi na kuongezea wale ambao tayari wamekuwa nao. 

"Baada ya juhudi tulizoweka kipindi cha kwanza, lazima kipindi kingefika ambapo tungechoka. Kwa bahati, tulibaki kwenye mechi na mganga mdogo akachipuka na kufunga bao ambalo labda ndilo kuu zaidi maishani mwake.

Ushindi huo uliwapa Liverpool uongozi wa alama mbili mbele ya Chelsea na kuwaweka alama saba mbele ya Manchester City, walio na mechi mbili ambazo hawajacheza. Ushindi katika mechi nne walizobaki nazo utawatunuku taji lao la 19 la Uingereza. 

Hisia za Gerrard mwisho wa mechi ya Jumapili zilikuwa wazi na anatumai kwamba ataendelea na msukumo huo kwenye mechi zilizosalia za Liverpool - ugenini Norwich City, nyumbani dhidi ya Chelsea, ugenini Crystal Palace na mwishowe nyumbani Anfield dhidi ya Newcastle United. 

"Safari ambayo nimekuwa nikisafiri miaka hiyo yote, kumekuwa na kupanda na kushuka. Kwa sasa, nafurahia kila kitu,” akasema.
“Najihisi kuwa na miaka 21 tena, nikicheza na wachezaji hawa nyota. Huenda huu ukawa mwezi mkuu zaidi katika uchezaji wangu. Nitajitolea kwa hali na mali.” 

"Ujumbe sasa ni kutulia na kuendelea kupambana – bado kuna fainali nne za kombe ambazo zimebaki.”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!