Searching...
Image and video hosting by TinyPic
15 April 2014
Tuesday, April 15, 2014

KUELEKA ARSENAL VS WESTHAM PALE EMIRATES



Na Oscar Oscar Jr
+255789784858

Thomas Vermaelen anasisitiza kwamba Arsenal wataweka kando athari za ushindi wao wa nusufainali Kombe la FA dhidi ya Wigan kwa wakati na kuangazia kufufua juhudi zao za kumaliza katika nne bora Ligi ya Premia. 

Timu ya Arsene Wenger ilisukumwa hadi ukutani na mabingwa watetezi Wigan na walihitaji bao la kusawazisha dakika za mwisho kutoka kwa Per Mertesacker kulazimisha kuchapwa kwa mikwaju ya penalti ambapo waliweza kuwabandua wapinzani wao wagumu baada ya sare ya 1-1 uwanjani Wembley Jumamosi. 

Wachezaji kadha wa Wenger walikuwa wakihangaishwa na uchovu muda wa ziada, huku beki wa kushoto Nacho Monreal akichechemea kipindi cha pili, lakini hakuna muda wa kupumzika vyema kwa Gunners, ambao lazima wawachape wapinzani wao wa London West Ham uwanjani Emirates Jumanne ili kuzidi kuwinda nafasi ya kushiriki Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. 

Everton waliwapita Gunners na kuchukua nafasi ya nne wikendi na timu hiyo ya Roberto Martinez ina nafuu ya alama mbili wakiwa wamebaki na mechi tano. 

Ushindi dhidi ya WestHam utawawezesha Arsenal kurejea nambari nne, japo kwa muda, kabla ya Everton kuwakaribisha Crystal Palace Jumatano, na difenda Mbelgiji Vermaelen anaamini kupewa motisha na kufika fainali ya Kombe la FA mara ya kwanza tangu 2005 – watakutana na Hull Wembley Mei 17 – kunaweza kufanya wachezaji wake wasahau uchovu mechi hiyo nyingine muhimu. 

“Ilikuwa siku ndefu na kujikwamua, lakini tumefanya hayo awali, kucheza Jumamosi na Jumanne, hivyo hatuwezi kutumia hicho kama kisingizio,” akasema Vermaelen. 

"Wengi waliongea kuhusu hitaji la ushindi kwa sababu tofauti, kwa meneja na kuonyesha kwamba tunaweza kupigana na nafikiri tulifanya hilo. 

“Ushindi huo utatupa motisha kwa kipindi kilichosalia cha msimu sasa. Tunaweza kusonga mbele kwa imani.
“Nina furaha sana kwamba tutaenda fainali,hiyo ndiyo sababu ya kucheza mechi hizi. 

“Ilikuwa mechi ngumu yenye muda wa ziada na penalti, huwa si rahisi lakini ulikuwa ushindi mzuri.”
Shangwe kutoka kwa wachezaji wa Arsenal na mashabiki baada ya mikwaju ya penalti zingefaa sana fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya au mechi ya kuamua mshindi wa Ligi ya Premia. 

Lakini nyuso hizo zenye furaha tele zilificha kupumua kwao kwa kuepuka kichapo kingine cha aibu msimu ambao ulionekana kuwa wa ahadi kuu lakini ulioonekana kutibuka kwa njia ya kushangaza huku Arsenal wakipambana kubandua wapinzani hao waliotoka ligi ya daraja la pili.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!