Searching...
Image and video hosting by TinyPic
8 April 2014
Tuesday, April 08, 2014

KUELEKEA YANGA VS KAGERA SUGAR KESHO TAIFA



 Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Young Africans kesho itashuka dimbani kucheza na wakata miwa kutoka mjini Bukoba timu ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara mzunguko wa raundi ya 24, kipute kitakachofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kikosi cha kocha mholanzi Hans Van der Pluijm kitaingia uwanjani kikiwa na kumbukumbu ya ushindi mnono wa mabao 5 - 1 mwishoni mwa wiki dhidi ya Maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini JKT Ruvu na kufikisha pointi 49 ikiwa ni ponti ne nyuma ya wanaongoza msimamo wa Ligi Azam FC.

Baada ya mchezo wa mwishoni mwa wiki dhidi ya JKT Ruvu, kikosi cha Young Africans jana jioni kiliingia kambini mjini Bagamoyo na kufanya mazoezi jana na leo asubuhi kwenye Uwanja wa Boko Beach Veteran eneo la Boko.

Kuelekea mchezo huo wa kesho Kocha Mkuu Hans amesema vijana wake 20 walioingia kambini wote wapo kwenye hali nzuri, kiafya, kifikra na morali ya kusaka pointi 3 ni ya hali ya juu kwani vijana wanahitaji kutetea Ubingwa tena kwa msimu wa pili mfululizo.

Katika mchezo wa awali uliozikutanisha Kagera Sugar na Young Africans katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Young Africans iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 wafungaji wakiwa ni Mrisho Ngasa na Hamisi Kizza.

Wachezaji Haruna Niyonzima, David Luhende, Athuman Idd, Emmanuel Okwi waliokuwa wagonjwa wanaendelea vizuri na watarajiwa kuungana na wenzao mara baada ya mchezo dhidi ya JKT Ruvu pamoja na mlinzi Kelvin Yondani aliyekua na kadi 3 za njano.

TAARIFA HII NI KWA MUJIBU WA WEBSITE YA YANGA

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!