Searching...
Image and video hosting by TinyPic
8 April 2014
Tuesday, April 08, 2014

MASHABIKI WA GUNNERS WAMTAKA WENGER KUSTAAFU .




 Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Baadhi ya mashabiki wa Arsenal wanataka meneja wao wa muda mrefu, Arsene Wenger, astaafu wadhifa wake mwisho wa musimu huu. 

Magwiji hao wa Uingereza waliendelea kushuka hadhi baada aya kunyukwa 3-0 na Everton kwenye ligi ya Premier ya Uingereza kuendeleza matokeo mabaya ya hivi majuzi. 

Wimbo unaorindima ndani ya mioyo ya mashabiki wa klabu hiyo ni kuwa wakati umewadia kwa mwalimu wao mkongwe kung'atuka madarakani baada ya kuwatumikia kwa miaka zaidi ya 18. 

Mashabiki wanamlaumu Wenger naye, kocha huyo anakilaumu kikosi chake kwa matokeo duni ambayo yamechangia kusalimisha uongozi wa Premier, kuondolewa kutoka ligi ya mabingwa na tishio la kumaliza miongoni mwa nne bora kwenye shindano kuu la Uingereza kwa mara ya kwanza katika miaka 16. 

"Lililobaki kwa silimia 100 tutang'ang'ania nafasi ya nne ingawaje ni vigumu," Wenger alisema.

Wenger ambaye amedumu katika wadhfa huo katika mechi 1003 amewahi kuingoza timu hiyo ya Uingereza kufuzu kwa mashindano 16 ya kombe la mabingwa barani Ulaya. 

Shabiki mmoja ameuliza katika mtandao wa Twitter kuwa iweje January walikuwa nambari moja, february nambari 2, Mwezi wa tatu 3 na sasa mwezi wa nne nambari nne? 

Mwingine asema Bwana Wenger amemtetea kwa miaka mingi - tisa kwa idadi -lakini leo amekoma.
Amejiunga na wale ambao wameanzisha kampeni katika mtandao Wenger ajiuzulu. 

Kilio cha Arsenal ni furaha ya Liverpool ambao baada ya kuitandika West ham 2-1 wametulia kileleni mwa ligi.
Bashasha sasa pia zasikika katika kambi iliyokuwa imefifia ya Manchester United baada ya kuimwagia machungu yao yote Newcastle 4- 0. 


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!