Searching...
Image and video hosting by TinyPic
8 April 2014
Tuesday, April 08, 2014

KUELEKEA CHELSEA VS PSG PALE DARAJANI



Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Chelsea wanabebwa na historia ambapo,wanasifa ya kuziondoa timu za Ufaransa lakini,wanakutanan na mtihani mzito mbele ya wababe wa Ligi 1 klabu ya Paris Saint-Germain, ambao mchezo wa awali,waliibuka kwa ushindi wa 3-1 kwenye michuano hiyo ya robo fainali ya klabu bingwa Ulaya. 

Chelsea wameruhusu wavu wao kuguswa mara moja tu kati ya safari tano ambazo wamekutana na wapinzani kutoka Ufaransa lakini,Jose Mourinho atakutana na mtihani mzito pale atakapowavaa  PSG, ambao wamefunga jumla ya mabao 14 kwenye mechi zao nne za ugenini msimu wa 2013/14 huku wababe hao wa Ufaransa wakiwatembelea kwenye jiji la London wakiwa mbele kwa mabao 3-1. 

PSG watakuwa bila mshambuliaji wao hatari Zlatan Ibrahimovic, ambaye aliumia mechi iliyopita na ambaye amefunga magoli kumi kwenye shindano hilo.Ibra amewahi kufanya kazi chini ya Mourinho msimu wa 2008/09 wote wakiwa Inter Millan.



Chelsea wanaelekea kwenye mchezo wao na PSG kujaribu kujipatia nafasi yao ya kwenda nusu ya fainali ya michuano hiyo kwa mara ya 7 katika awamu 11 ambazo wameshiriki michuano hiyo.Walifanikiwa kutinga katika hatua hiyo kwa kuwafunga  2-0 nyumbani timu ya Galatasaray AS, kwenye hatua ya 16 bora.


.
Chelsea wameshinda mechi zao saba kati ya kumi na mbili za mashindano ya Uefa ambapo,walikuwa wamepoteza mchezo wao wa kwanza na kupindua matokea wanapokuwa uwanja wao wa nyumbani pale Stamford Bridge,na hivi karibuni tumeshuhudia wakifanya hivyo dhidi ya timu ya Steaua Bucuresti msimu uliopita kwenye Europa League hatua ya 16 bora  baada ya kufungwa ugenini 1-0 na walipokuja darajani,wakashinda 3-1.

Lakini pia walifanikiwa kuwaondoa  Napoli kwa mabao  4-1 baada ya muda wa nyongeza msimu wa 2011/12 kwenye hatua ya 16 bora ya klabu bingwa Ulaya baada ya kuwa wametandikwa  3-1 mechi ya kwanza ugenini na baada ya hapo,walikwenda na kutwaa ubingwa wa michuano hiyo

Lakini pia kwa upande wa pili,wamewahi kupoteza kwa mabao 3-1 ugenini dhidi ya timu ya Monaco na kwenye mechi ya marudiano,ikamalizika kwa timu hizo kufungana kwa mabao  2-2 msimu wa  2003/04 kwenye nusu fainali za klabu bingwa Ulaya wakiwa nyumbani.


PSG wametinga robo fainali kwa mara ya pili mfululizo na kwa mara ya tatu katika historia.Mwaka jana waliweza kutoka sare ya 2-2 dhidi ya klabu Barcelona wakiwa nyumbani Ufaransa na mechi ya marudiano,ilimalizika kwa sare pia ya bao 1-1 pale Camp Nou,na kusukumwa nje kwa sheria ya goli la ugenini.


PSG wameshinda mechi zao sita kati ya kumi na moja za hivi karibuni za ligi ya mabingwa Ulaya na kupoteza mechi mbili tu.Nusu fainali yao nyingine ilipatikana baada ya kupata ushindi kwa uwiano wa mabao 3-0 dhidi ya AC Milan msimu wa 1994/95. 

Timu hizo zitakutana baadae pale London na kila mmoja akihitaji nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!