Searching...
Image and video hosting by TinyPic
2 April 2014
Wednesday, April 02, 2014

PEP GAUDIOLA:REFA ALIEGEMEA UPANDE WA MAN UNITED



Kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola, alionyesha dalili za kutatizwa na mabingwa wake wa kombe la mabingwa Ulaya, Bayern Munich, kushindwa kuwapiku Manchester United waliowalazimisha kutoka sare ya 1-1 uwanjani Old Trafford kwenye mkondo wa kwanza wa robo fainali yao.

Bastian Schweinsteiger alifuta bao la ufunguzi kutoka kwa kapteni Nemanja Vidic wa United kuongoza Bayern kudhibiti mchuano huu ingawa kiungo huyo alipata kadi nyekundu muda ukiyoyoma na hivyo hatocheza kwenye patashika ya marudiano.

Beki wa kati, Javi Martinez, pia atakosa mechi ya Aprili 9 kwenye uwanja wa Bayern, Allianz Arena baada ya kulamba kadi ya njano kwa kumchezea Javier Hernandez, visivyo. 

Baada ya mechi hiyo, Guardiola alimsuta mwamuzi wa Uhispania, Carlos Velasco Carballo, kwa tuhuma za kuegemea zaidi upande wa United.
“Nilizungumza na refa na anafahamu maoni yangu. Alinipa yake na kunikumbatia kwa hima na nitamtakia safari njema akirudi Uhispania,” mwalimu huyo aliambia wanahabari. 

Alipoulizwa ikiwa alikubaliana na raia mwenzake wa Uhispania kumtoa Schweinsteiger uwanjani, kocha huyo alijibu kwa dhati, “Hapana kabisa.”
“Nadhani yeye ni refa mzuri na alichezesha mchezo mzuri lakini uamuzi huo haukuwa wa haki. Hewala, kushinda kombe la mabingwa, ni lazima umudu chochote unachokumbana nacho na mara nyingine, haya hutokea,” Guardiola aliongeza.

Kocha huyo aliyeongoza Barcelona kunyakua kombe hilo mara mbili kisha alijibizana na ripota wa Uingereza aliyetaka kujua ikiwa alionelea kuwa United walicheza mchezo hasi. 

“Sikusema hivyo, naheshimu mwenzangu (meneja wa United David Moyes). Nikizungumza nawe, nitizame, usiangalie pengine ili unielewe,” Guardiola, aliyepandwa na hasira alisema. 

Licha ya kutawala mchezo huo, Bayern hawakufanikiwa kubuni nafasi nyingi za wazi, jambo ambalo litampa Guardiola changamoto kabla ya marudiano.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!