Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 March 2014
Thursday, March 20, 2014

WALETENI,ASEMA MOURINHO.


Jose Mourinho amesimama wima na kutangaza kuwa klabu yake Chelsea haiogopi kumenyana na yeyote baada ya vijana wake kufuzu robo fainali ya Champions League bila kutoa jasho.
Magwiji hao wa Uingereza walilaza Galatasary wa Uturuki 2-0 Jumanne usiku katika uwanja wa Stamford Bridge na kukamilisha ushindi wa 3-1 kwa jumla baada ya mikondo miwili ya mechi yao ya raundi ya 16-bora. 

Mabao katika kipindi cha kwanza kutoka Samuel Eto’o na Gary Cahill yalikamilisha ushindi huo rahisi huku Galatasaray wakikosa jibu.
Chelsea wanakodolea changa moto iliyoko mbele yao ya kukutana na miamba wa bara la Ulaya ikiwemo mabingwa watetezi, Bayern Munich, Barcelona, Real Madrid na Paris St Germain ambao pia wamejikatia tiketi za robo fainali. 

“Timu zote kubwa zimefuzu na tunazikaribisha kwa mikono miwili. Itakuwa ni jambo bora kujipima na miamba hao ili kudhihirisha maendeleo yetu. Tunangoja droo kwa hamu,” mwalimu huyo mwenye mbwembwe alitangaza. 

Viungo nyota, Eden Hazard, Oscar na Willian ambao wameshamiri msimu huu, watacheza kwa mara ya kwanza katika awamu hiyo ya shindano la mabingwa huku ari yao pamoja na meneja mwenye uzoefu ikijumuika kuwapa Chelsea matumaini makuu.

Tayari, mwalimu huyo wa Ureno ameongoza Porto na Inter Milan kunyakua taji hilo na anatazamia kuandikisha historia mpya kwa kushinda na klabu yake ya tatu.
Droo itafanyika Ijumaa.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!