Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 March 2014
Thursday, March 20, 2014

LAMPARD AFURAHIA MWENDO WA CHELSEA



Frank Lampard ana furaha sana kuona Chelsea ikiwa  kileleni mwa Ligi ya Premia baada ya misimu kadha ambayo wamekuwa hawafanyi vyema.
Mwaka 2005, Jose Mourinho aliongoza klabu hiyo ya London kushinda taji la kwanza katika miaka 50 na wakalitetea msimu uliofuata.
Hata hivyo, The Blues wameshinda taji moja pekee la ligi hiyo tangu wakati huyo, mwaka 2010 chini ya Carlo Ancelotti.

Chelsea walishinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2012 na Kombe la FA lakini wakamaliza alama 25 nyuma ya washindi Manchester City wakiwa nambari sita.
Mwaka mmoja baadaye walimaliza nambari tatu na alama 14 nyuma ya washindi Manchester United, lakini wakashinda Europa League.

Mourinho, aliyerudi Stamford Bridge kabla ya mwanzo wa msimu huu, amepuuzia mbali uwezekano wa Chelsea kushinda taji, akisema anapigia upatu Manchester City ambao wana mechi tatu za kucheza washinde.

Lakini kiungo wa kati wa Uingereza Lampard, ambaye timu yake ilipata pigo kwa kushindwa 1-0 na Aston Villa wikendi iliyopita, hata hivyo amesema anafuraha kuona Chelsea wakiwa alama nne mbele ya Liverpool.
"Ni jambo zuri sana kuwa hapo,” Lampard alisema.
“Tumekuwa na miaka kadha, miwili au mitatu ambayo tumekuwa nyuma sana,” akaongeza kiungo huyo wa kati wa Uingereza.

“Ni vizuri sana kurudi tena kupigania taji na kuhisi hilo kwenye klabu, kuhisi kwamba mnapigania taji na si kumaliza katika nne bora. Ni jambo zuri sana.”
Baada ya kufika robofainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa ushindi wa jumla wa 3-1 dhidi ya Galatasaray, Chelsea watacheza debi ya London dhidi ya Arsenal – ambao wanatafuta taji la kwanza baada ya miaka tisa ya ukame.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!