Kiungo wa Real Madrid Jese hatoshiriki mechi yeyote msimu huu baada ya kujeruhiwa vibaya katika mechi hiyo dhidi ya Shalke 04.
Jesse mwenye umri wa miaka 21 alianguka vibaya baada ya makabiliano
na beki wa Schalke Sead Kolasinac na akalazimika kubebwa kwenye machela
daktari akisema ni jereha la goti.
Kocha wa klabu hicho tajiri duniani Carlo Ancelotti amedhibitisha
kuwa Jesse ameumia kiasi cha kuwa amefunga msimu na kuwa klabu hiyo itamsaidia katika matibabu ya jeraha hilo la goti hadi atakaporejea
msimu ujao.
Jesse ameichezea Madrid katika mechi 31 na kuifungia mabao nane, la
kwanza likiwa bao dhidi ya mahasimu wao wa jadi Barcelona mwaka
uliopita.
Kutokana na ushindi huo mkubwa Madrid sasa inajiunga na Barcelona na
Athletico Madrid katika droo ya hatua ijayo ya robo fainali
inayotarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa.
Real vilevile inatarajia kuendeleza msururu wa matokeo mema katika
ligi yao ya nyumbani La liga ambapo imeratibiwa kukwaruzana na watani
wao wa jadi Barcelona siku ya Jumapili katika mechi inayotizamiwa na
mashabiki wengi zaidi duniani ya El -Classico.
0 comments:
Post a Comment