Searching...
Image and video hosting by TinyPic
6 June 2013
Thursday, June 06, 2013

UNITED INATAKIWA KUNUNUA WINGA WAPYA



NIONAVYO MIMI kwa mawinga wa UNITED.

Antonio Valencia
huyu ni winga wa kulia wa united na Ecuador,amekuwa haeleweki kama homa za vipindi.Kuna muda akikosekana united inayumba na kuna muda anaharibu sana mashambulizi ya united.Kazaliwa mwaka 1985,nadhani angepisha tu.

Ashley Young                                          


huyu ni winga na kiungo wa united na Uingereza kazaliwa 1985,nadhani hana jipya tangu ajiunge na united.Amekuwa akijiangusha na kupiga krosi fyongo kila siku.Kama vipi arudi alikotoka,Moyes anatakiwa kutafuta mbadala wake.

Luis Nani                                      

Nadhani huyu jamaa kashindwa kuziba nafasi ya Ronaldo,uwezo wake wa kuwahadaa mabeki siku hizi hauonekani na mbio zake hazina msaada kwa united. Nadhani viungo wa united wa sasa,hawamchezeshi vizuri.Bado anauwezo kazaliwa 1986 ila akiendelea kusubiri pasi za Clevery na Anderson,atafulia.

Ryan Giggs                                   

ulejendari nao ukipitiliza yaweza kuwa matatizo,tunajua kama anaipenda united na kaisaidia vya kutosha lakini hana jipya tena.Giggs kazaliwa 1973 nadhani anahitajika zaidi benchi la Ufundi na sio uwanjani sio kwa umri tu,uwezo pia umepungua.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!