taifa stars
NIONAVYO MIMI KWA TAIFA STARS
Kocha Kim Poulsen amejitahidi sana kuitengeneza timu yetu ya Taifa na kurudisha mashabiki wengi ambao walikuta wameshakata tamaa.Hakuna shabiki ambaye anapenda timu yake ifanye vibaya kila siku.KAMA TANGU UJIO WA MAXIMO lengo letu lingekuwa sio kushinda bali kuandaa timu ya kwenda BRAZIL mwakani,basi kuna uwezekano mkubwa sana tungefanikiwa.
Sitaki kusema kwamba kwa sasa hatuwezi kwenda BRAZIL NO,tunaweza lakini tunanafasi kidogo sana ya kwenda ingawa tunashika nafasi ya pili kwenye kundi letu.Kuwapa motisha wachezaji wetu ni jambo zuri lakini linatakiwa kuwa endelevu hata kama hatutakwenda BRAZIL.
Kwanamna vijana wetu wanavyocheza soka,nadhani tulitakiwa kuwa na wachezaji hata wanne wakicheza KENYA na UGANDA huku tukiwa na wengine waliosambaa BURUNDI,RWANDA,MALAWI na kwingineko Africa kabla ya kwenda Ulaya wenye umri mdogo na kiwango bora.
Nadhani kwa sasa tunavuna matunda ya SAMATTA na ULIMWENGU,tunahitaji kuwanao wengi wa aina hii ili kuongeza ubora kwenye kikosi chetu.Mimi binafsi nina asilimia chache sana za sisi kwenda BRAZIL lakini najua msimu ujao kama mfumo huu utakuwa endelevu,MATAIFA YA AFRICA tutakwenda.
0 comments:
Post a Comment