Searching...
Image and video hosting by TinyPic
11 June 2013
Tuesday, June 11, 2013

AMR KIEMBA ASAINI MKATABA MIAKA MIWILI MBELE KUUZWA MOROCCO

                                                  


Klabu ya Simba ya Dar es Salaam imetangaza kufikia makubaliano ya kuongeza mkataba na kiungo anayesadikiwa kua bora kabisa kwa sasa Tanzania Amri Kiemba.

Mchezaji huyo ambaye alicheza vizuri sana dhidi ya Morocco huku akitupatia bao pekee alilofunga kwa ustadi mkubwa hata kufanya klabu za Morocco kuanza kutaka mazungumzo ya kumsajili kiungo huyo kitu ambacho Simba wameshaanza kukichangamkia. 

Mara baada ya kurejea kutoka katika mchezo dhidi ya Morocco jana Simba ilikuwa kwenye jitihada nzito kuhakikisha inamzuia Kiemba kusaini Yanga kwa kumpa ofa nono ya mkataba mpya, Kiemba alikuwa akihitaji kiasi cha millioni 38 ili asaini msimbazi lakini baada ya mazungumzo marefu Kiemba amekubali kusaini kwa kiasi cha millioni 35 kwa miaka miwili.

Pia Kiemba atakuwa analipwa mshahara wa millioni 2 kwa mwezi. Alisaini mkataba huo mbele ya kaimu makamu mwenyekiti Mzee Kinesi.

Mkurugenzi wa masuala ya usajili Simba akiongea kutokea Arabuni alipokwenda kufuatilia pesa za ada ya uhamisho wa aliyekua mchezaji wa klabu hiyo Emmanuel Okwi alithibitisha kwenye redio fulani hapa Dar es Salaam kwamba Simba nia yao ni kumuuza na hata mkataba walioingia nae ni kwa kua wana uhakika wa kumuuza huko Arabuni.

Pia alidai ameshapokea mualiko wa kwenda kulizungumzia suala la uhamisho wa Kiemba huko Morocco na baada ya kumaliza masuala ya pesa za usajili za Okwi atarejea Morocco kwa suala la Kiemba.

Unadhani ni vizuri kumuuza ili kupata fedha zitakazojenga timu zaidi au kumtumia kwa msimu huu ili kurudisha heshima yao?

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!