KLABU ya Manchester United iko karibu kabisa kumsajili kiungo wa Barcelona, Thiago Alcantara kwa dau la Pauni Milioni 17.
Mabingwa
hao wa Ligi Kuu ya England wamewapiku wapinzani wao, Manchester City
kwa kukubaliana juu ya maslahi binafsi na mchezaji huyo mwenye umri wa
miaka 22, ambaye watakuwa wanamlipa Pauni Milioni 5 kwa mwaka.
Makubaliano yamemhusisha Thiago na baba yake, Mazinho.
Sasa
wanatakiwa kumalizana na Barcelona na vyanzo vinasema habari rasmi
inaweza ikatolewa leo, lakini majadiliano baina ya klabu hizo mbili
yataendelea mwishoni mwa wiki.

Anakuja: Thiago Alcantara yuko njiani kuelekea Manchester United

Thiago
akimkabidhi Waziri Mkuu wa Hispania, Mariano Rajoy (kulia) jezi
aliyoisaini ya timu ya vijana ya Hispania chini ya umri wa miaka 21
baada ya kutwaa ubingwa wa Ulaya
Thiago
anatazamwa kama mmoja wa nyota wanaochipukia katika soka ya Hispania na
alionyesha makali yake alipofunga Hat-trick wakati U-21 inatwaa ubingwa
wa Ulaya wiki hii.
Lakini amekuwa hana furaha kwa kukosa nafasi Nou Camp, licha ya Barca kumuhakikishia atakuwa kinara katika timu yao baadaye.

Kipaji: Barcelona wanatumai kiungo huyu atakuwa tegemeo lao baadaye

Mstaafu: United inahitaji mrithi wa muda mrefu wa Paul schoels
0 comments:
Post a Comment