Meck Mexime apasua jipu!
Na Oscar Oscar Jr
Baada ya kuongoza ligi kwa muda mrefu pasipo kupoteza mchezo wowote, timu ya Mtibwa Sugar inaonekana kutetereka kwa sasa baada ya kufungwa mechi nne mpaka sasa huku ikichezea pia kipigo kikubwa msimu huu kutoka kwa Azam cha mabao 5-2.
Kocha wa timu hiyo, Meck Mexime amezungumza jioni ya leo na kituo cha EFM kwenye kipindi cha E-Sports na kueleza kuwa wachezaji wake wanaonekana kupagawa kwa sasa.
Mexime amezungumza kuwa pamoja na kufanya maandalizi sahihi kwenye kikosi chake, bado vijana hao wamepoteza hali ya kujiamini na kujikuta wakipokea vichapo tu kila wanaposhuka dimbani.
Kabla ya Mtibwa Sugar kwenda kwenye michuano ya Mapinduzi, walikuwa wanaongoza ligi huku washambuliaji wake Ame Ally na Ally Shomari wakitawala vichwa vya magazeti hapa nchini kila siku kutokana na umahiri wao.
Baada ya kupoteza mchezo wao wa fainali dhdi ya Simba kwa changamoto ya mikwaju ya Penalty, timu hiyo imeporomoka na sasa wanakamata nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara wakiwa na pointi 19.
Meck Mexime anapaswa kufanya mabadiliko ya kiufundi mapema kwa sababu alama 19 sio salama kwake hususani kwenye ligi ya mwaka huu ambayo timu inaposhinda mechi tatu, inakuwa kwenye nafasi za kuwania ubingwa na inapopoteza mechi kama hizo, inakuwa kwenye timu zinazopiga kukweka kushuka daraja.
0 comments:
Post a Comment