Na Chikoti Cico
.
Klabu
ya Chelsea yenye maskani yake jijini London imetupwa nje ya michuano ya
kombe la FA kwenye raundi ya nne kwa “aibu” baada ya kuchapwa kwa
magoli 4-2 dhidi ya Bradford City inayoshiriki ligi daraja la kwanza
nchini Uingereza.
Katika mchezo huo Chelsea ndiyo walikuwa wa kwanza kuliona lango la Bradford kwenye dakika ya 22 ya mchezo ambapo Gary Cahill aliunganisha mpira wa kona uliochongwa na Oscar na kuiandikia Chelsea goli la kwanza, na wakati mchezo ukikaribia kwenda mapumziko Ramires aliipatia Chelsea goli la pili baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mohamed Salah.
Kwenye dakika ya 41 kabla yakipindi cha kwanza kuisha Jon Stead aliipatia Bradford goli na kufanya mpaka wakati timu zinakwenda mapumziko matokeo kuwa 2-1 kwenye uwanja wa Stamford Bridge.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Chelsea wakilinda magoli yao mawili huku Bradford wakitafuta goli la kusawazisha na kwenye dakika ya 75 Felipe Morais aliipatia Brardford goli la kusawazisha.
Goli ambalo liliamsha ari ya wachezaji wa timu hiyo na huku mpira ukielekea kuisha Halliday aliipatia timu hiyo goli la tatu kwenye dakika ya 81 kabla ya Yeates kukamilisha “aibu” ya Chelsea kwa kufunga goli la nne kwenye dakika ya 93.
Hivyo mpaka mwisho wa mchezo huo ubao wa magoli ulisomeka Chelsea 2-4 Bradford, matokeo yaliyopelekea Chelsea kutupwa nje ya raundi ya nne ya kombe la FA na hivyo ndoto za kocha wa Chelsea Jose Mourinho kunyakua makombe manne msimu huu yaani “quadruple” kuota mbawa.

0 comments:
Post a Comment