Arsenal na dirisha la usajili.
Na Oscar Oscar Jr
Klabu ya arsenal tayari imeanza mazungumzo rasmi ya kumuwania Kiungo wa Borussia Dortmund, Ilkay Gundogan huku kiasi ya Pauni 16M zikitajwa kuhitajika katika usajili huo.
Arsenal wamekuwa na tatizo la kiungo mkabaji kwa muda sasa tangu kuondoka kwa Alex Song aliyetimkia Barcelona na nafasi hiyo kucheza na Aaron Ramsey, Mikel Arteta na Methew Flamin huku wote wakionekana kupwaya.
Pamoja na kufanya mazungumzo ya kumnasa kiungo huyo, Gunners wametajwa pia na magazeti ya leo barani Ulaya kumuhitaji mshambuliaji wa klabu ya PSG, Ednison Cavani ambaye anaonekana kuto ridhika na namna mambo yanavyoendelea kwa mabingwa hao wa Ufaransa.
Kumpata Cavani kutaongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya Arsenal inayoongozwa na Alexies Sanchez ambaye amefunga magoli 10 ya ligi kuu mpaka sasa.
Kwa upande mwingine, Arsenal wanaonekana kumuwinda kipa wa Chelsea Peter Cech na kula dalili za kumpata baada ya msimu huu kumalizika.
Arsenal kwa sasa wanakamata nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza wakiwa na alama 33 na wikendi hii watakuwa dimbani Emirates kuvaana na Stoke City majira ya saa 10:30 Jioni.
0 comments:
Post a Comment