Na Chikoti Cico
Stoke City wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Britania, watawaalika timu ya Arsenal kwenye moja ya mechi za ligi kuu nchini Uingereza katika kutafuta alama tatu muhimu, Refa Anthony Taylor ndiye atakayechezesha mchezo huo.
Stoke City inayofundishwa na kocha Mark Hughes, bado inakabiliwa na wachezaji mengi majeruhi na kuelekea kwenye mchezo huo itawakosa Steve Sidwell, Peter Odemwingie, Victor Moses, Glen Whelan na Dionatan Teixeira ambao ni majeruhi.
Baada ya kupoteza michezo mitatu mfululizo huku wakiwa na alama 15 na kushika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi kuu, timu ya Stoke inahitajika kupigana kufa na kupona kuifunga Arsenal ili kujiweka kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi hasa ikizingatiwa kwamba, mchezo huo utafanyikia kwenye uwanja wao wa nyumbani.
Kuelekea mchezo huo, takwimu zinaonyesha Stoke wamekuwa na rekodi nzuri dhidi ya Arsenal kwenye uwanja wa Britannia kwani katika michezo nane waliyocheza wameshinda michezo minne, wametoka sare michezo mitatu na kufungwa mchezo mmoja peke.
Kwa upande mwingine, takwimu zinaonyesha mshambuliaji wa Stoke, Peter Crouch ameifunga Arsenal goli saba kwenye mechi mbalimbali alizokutana nao.
Kikosi cha Stoke City kinaweza kuwa hivi: Begovic; Bardsley, Shawcross, Wilson, Pieters; Cameron, N'Zonzi; Assaidi, Bojan, Arnautovic; Diouf
Kwa upande wa timu ya Arsenal nao pia wanasumbuliwa na wachezaji wengi ambao ni majeruhi kuelekea mchezo huo. Watawakosa Mathieu Debuchy, Theo Walcott, Mikel Arteta, Mesut Ozil, David Ospina, Abou Diaby, Jack Wilshere na Nacho Monreal.
Wakiwa na alama 23 na kushika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi, timu ya Arsenal inayofundishwa na kocha Mfaransa, Arsene Wenger wanatarajiwa kuendeleza wimbi la ushindi baada ya kushinda mechi mbili zilizopita hivyo kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kurejea katika nne nafasi za juu (top four).
Kikosi cha Arsenal kinaweza kuwa hivi: Martinez; Chambers, Mertesacker, Koscielny, Monreal; Flamini, Ramsey; Welbeck, Cazorla, Sanchez, Giroud.
Rekodi za timu hizi mbili zinaonyesha katika michezo 86 waliyokutana kwenye ligi, Stoke ameshinda mara 23 huku Arsenal akishinda mara 43 na wametoka sare mara 20.
0 comments:
Post a Comment