DIEGO COSTA KUIKOSA MECHI YA LEO DHIDI YA BARCELONA.
Mshambuliaji wa kutegemewa wa timu ya Atletico Madrid,Diego Costa kuna hati hati ya kutocheza mechi ya leo dhidi ya Barcelona kwenye hatua ya robo fainali ya klabu bingwa Ulaya kutokana na kupata maumivu na mchubuko kwenye goti lake la kushoto,kocha wa Atletico Diego Simeone aliwaambia wanahabari jana jumatatu.
"Kwa namna nilivyo muangalia kwenye mazoezi,nadhani anaweza kuwa tu kwenye hali nzuri ya kuanza katika mechi hiyo "aliongezea Simeone.
"Ingawa, tunalazimika kusubiri na kuona namna anavyoendelea kwa kuwa bado kuna masaa mengi mpaka mchezo huo kuanza."
Costa, 25, amekuwa mwiba hatari msimu huu akiwa na Atletico kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya na kwenye ligi ya Hispania La Liga.Aliumia siku ya jumamosi kwenye mchezo ambao ulimalizika kwa timu yake kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Athletic Bilbao ambapo alifunga goli la kwanza.
Kufuatia matokeo hayo, Atletico waliweza kuwa mbele ya Barcelona kwa lalama moja juu ya msimamo wa ligi.Kuelekea mchezo huo wa leo,Atletico watamkosa pia kiungo Raul Garcia ambaye anatumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja.
0 comments:
Post a Comment