Manchester United imepangwa kucheza na Bayern Munich
katika michuano ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya huku
Chelsea ikipangwa kukutana na Paris St-Germain.
Mabingwa wa ligi ya Uhispania, Barcelona
watapambana na Atletico Madrid, huku Real Madrid ikipangwa kukutana na
Borussia Dortmund.Mechi zao za mzunguko wa kwanza zitaanza tarehe 1 mpaka 2 mwezi Aprili na marudiano yatakuwa tarehe 8-9 Aprili.
Fainali ya michuano hiyo itapigwa katika uwanja jijini Lisbon wa Estadio da Luz tarehe 24 mwezi Mei.
Manchester na Bayern wanakutana tena tangu mwaka 1999 kwenye fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa, ambapo Ole Gunnar Solkjaer na Teddy Sheringham waliiwezesha Manchester kutwaa kikombe chini ya Kocha wao Alex Ferguson na kwa siku za usoni,walikutana mwaka 2010 ambapo,Bayern walifanikiwa kusonga mbele.
Mara baada ya kupangwa kwa timu hizo nchini Switzerland, beki kisiki wa Bayern, Philipp Lahm amesema kuwa hawawezi kutetereshwa na nafasi waliyonayo United kwa sasa katika ligi kuu na kusema kuwa watasafiri mpaka Manchester kwa kazi moja tu, nayo ni kufunga magoli.
Chelsea inayoongoza kwenye msimamo wa ligi itaifuata PSG nchini Ufaransa katika mzunguko wa kwanza.
0 comments:
Post a Comment