YANGA MWENDO MDUNDO
Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara Vodacom na mabingwa watetezi wa kombe la Kagame timu ya Young Africans imeendelea na mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kombe la Kagame 2013/2014.
Young Africans ambayo ilianza mazoezi tangu wiki iliyopita, inaendelea kuimarika kutokana na wachezaji wote kufanya mazoezi isipokua wachezaji waliopo katika timu za Taifa wakitumikia majukumu ya nchi zao.
Kocha Brandts akiongea mara baada ya mazoezi alisema anashukuru vijana wake wako katika hali nzuri, kikosi kinaendela kujifua na wachezaji wote wako fit kiakili, kiafya na hakuna majeruhi hata mmoja hivyo ni nafasi nzuri kwangu kuweza kutoa mafunzo kwa wachezaji wangu.
"Tumeanza mazoezi wiki iliyopita hapa hapa katika uwanja wa shule ya Sekondari Loyola, tunajianda na mashindano ya kombe la Kagame huku tukisibiria taarifa rasmi ya serikali juu ya usalama wa nchi ya Sudan, lakini pia tunatumia fursa hii kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom 2013/2014" alisema Brandts.
Aidha Brandts amesema kwa sasa anawakosa wachezaji wake zaidi ya nane waliopo katika timu za taifa kwa majukumu ya kuziwakilisha nchi zao lakini anaamini kufikia jumatatu ijayo wachezaji hao watakua wameshamaliza michezo yao na kujiunga na mazoezi ya klabu yao.
Mashindano ya Kagame mwaka hu yamepangwa kufanyika nchini Sudan katika majimbo ya Darfur - Kaskazini katika mji wa Al - Fashir na Kordufuan Kusini kwenye mji wa Kadugli kuanzia tarehe 18 Juni 2013.
Mapema mei 10 mwaka huu klabu ya Yanga ililiandikia barua Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) kuulizia juu ya hali ya usalama, malazi na huduma zote watakazopatiwa timu ya Yanga ikienda nchini Sudan, lakini mpaka serikali inatamka bungeni juu ya hali ya Sudan walikua bado hawajajibu barua hiyo
0 comments:
Post a Comment