Searching...
Image and video hosting by TinyPic
10 June 2013
Monday, June 10, 2013

HIGUAIN | MADRID BADO YAMTAKA, ARSENAL YAONGEA NA BABA YAKE, JUVE YAKIMBILIA KWA UONGOZI WA MADRID



                                                                     


Juventus wamestushwa na mwenendo wa Arsenal juu ya straika wa Real Madrid Gonzalo Higuain hivyo nao kupanga mashambulizi upya kuhakikisha wanamtia mikononi.

Klabu hiyo machampioni wa Itali walistushwa na habari kwamba meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekutana faragha na baba mzazi wa Higuain aitwaye Jorge ambaye ndiye kama ajenti wa mshambulizi huyo.


Wenger ameshaweka wazi kwamba hayuko tayari kumpoteza Higuain na ameshatayarisha dau linalofikia £19million kwa Muargentina huyo huku wakimtengea mshahara £150,000-kwa-wiki.
Siku ya Jumapili Juve walitumia vizuri fursa ya kukutana na Real Madrid walipohudhuria Bernabeu mchezo wa malejendari baina ya klabu hizo mbili ambao ulivuta mashabiki zaidi ya 80,000 hivyo kukutana na uongozi Real.

Rais wa Real Florentino Perez alifanya mazungumzo na rais wa Juve Andrea Agnelli, katika moja ya migahawa ya Bernabeu.
Juve wanahaha kumnasa Higuain ambaye ki-umri akiwa na miaka 25, ingawa ameshafanya makubwa lakini bado kuna mengi yanatarajiwa kutoka kwake.


Perez amesisitiza kwamba Real hawana nia ya kumuuza mchezaji huyo lakini kama mchezaji mwenyewe atataka kuondoka basi watamruhusu.
na inaonekana klabu zote mbili Arsenal na Juve wanaweza kutakiwa kusubiri meneja mpya wa Real Madrid — ambaye bado anatazamiwa kua Carlo Ancelotti — kama atahitaji huduma za Higuain.
Bosi huyo wa zamani wa Chelsea, ambaye bado anafukuziwa na Real kama kuchukua mikoba ya Jose Mourinho, anaweza kuamua kama Higuain auzwe au abaki.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!