SI Simba, Yanga na Azam tu, usajili umechanganya kwa klabu zote za Bara kujiandaa na Ligi Kuu itakayoanza Agosti.
Uongozi wa Coastal Union umetuma ofa Simba kumtaka
kwa mkopo winga wake wa zamani Uhuru Seleiman na Mkurugenzi wa Ufundi,
Nassoro Bin Slim amethibitisha hilo.
Alisema wapo katika hatua za mwisho kukamilisha
usajili wa straika wa Bandari ya Kenya, Crispian Odulla na mpaka sasa
wachezaji wao wapya ni Haruna Moshi, Juma Nyosso (Simba), Keneth
Masumbuko (Polisi Moro), Marcus Ndaheli, Said Rubawa (Oljoro JKT) na
Abdullah Othman (Jamhuri ya Pemba)
Mgambo JKT ya Tanga, kocha wao Mohammed Kampira
ameweka wazi kuwa wamemsajili straika mkongwe Salim Aziz ‘Gilla’
aliyewika na Simba pamoja na Coastal Union.
Oljoro JKT ya Arusha, Katibu wao Alex Mwamgaya
amesema bado wanatafakari kabla ya kuanza usajili wao rasmi kwa ajili ya
msimu ujao wa ligi.
Straika matata wa zamani wa Tanzania ambaye sasa
ni kocha msaidizi wa Prisons, Oswald Morris anasema bado wapo likizo
lakini wamependekeza kusajili wachezaji wapya tisa kwenye ripoti yao.
Mtibwa Sugar wamethibitisha wako kwenye mazungumzo na Yanga kumtaka beki wa kushoto Stephano Mwasika anayesugua benchi.
0 comments:
Post a Comment