KLABU ya Southampton imekubali kulipa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 10 kumnunua kiungo Mkenya wa Celtic, Victor Wanyama.
Watakatifu hao, ni miongoni mwa klabu
zinazoitaka saini ya Waynama – zikiwemo Arsenal, Liverpool na Inter
Milan – na sasa wanaingia katika orodha ya klabu zinazogombea saini
yake.
Mpenda kuambaa pembeni: Victor Wanyama anatakiwa na klabu kadhaa kubwa Ulaya
Yuko juu: Kung'ara kwa kiungo katika Ligi ya Mabingwa kumemfanya amulikwe na wengi
Kinda huyo wa umri wa miaka 21 amekuwa
mmoja wa wachezaji wakubwa wa Celtic tangu ajiunge na klabu hiyo ya
Scotland kutoka Beerschot ya Ubelgiji kwa Pauni 900,000 miaka miwili
iliyopita.
Lakini Wanyama amebakiza miaka miwili
katika Mkataba wake wa sasa na Celtic ambao hawatakuwa na chaguo zaidi
ya kukubali faida kumuuza.
0 comments:
Post a Comment