NIONAVYO MIMI KATIKA TETESI ZA REAL MADRID.
Uongozi wa madrid amepanga kuvunja Rekodi kwa kumuandalia CR7 £155m ili aendelee kubaki katika club hiyo na kusaini mkataba wa miaka 5.Nadhani Madrid wanakila sababu yakumpa CR7 anachotaka.
2.Carlo Anceloti inadaiwa tayari amefikia makubaliano ya kuifua timu ya Real Madrid akitokea PSG na atatangazwa rasmi tarehe 3 July.Huyu ni kocha ambaye mimi namuhusudu sana na Real Madrid nadhani safari yao ya UCL ubingwa wa 10 unanukia.
Gonzalo Higuain huenda akakimbia Santiago Bernabeu na kutua Emirates kwa ada ya £22m. Edison Cavvan na Luiz Suarez wanatajwa kwenda Real Madrid kuziba nafasi yake.
Isco kwenda Madrid inasemekana dili limeshakamilika na atatangazwa baada ya michuano ya U21 kamalizika.Ingawa man city nao wanamtolea macho.
Gareth Bale dili linaonekana litachelewa kidogo lakini Madrid wanasema atakuwa mchezaji wao rasmi kabla ya July 28 ambapo Real Madrid wataelekea ziarani Marekani.Wanataka kwenda na Bale Marekani.
0 comments:
Post a Comment