Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 January 2017
Monday, January 30, 2017

IVANOVIC KUTIMKA CHELSEA


Na FLORENCE GR

Kocha wa klabu ya soka ya Chelsea muitaliano Antonio Conte amethibitisha kuwa mchezaji Branislav Ivanovic yupo katika mazungumzo na klabu mbalimbali ilikukamilisha usajili wake kabla ya dirisha la usajili halijafungwa siku ya kesho.

Ivanovic amekuwepo kwenye timu hiyo tangu mwaka 2008 ambapo amefanikiwa kushinda mataji mawili ya EPL, makombe matatu ya FA, europa ligi,klabu bingwa barani ulaya na kombe la ligi mara moja.

Mchezaji huyo ambaye amekuwa na wakati mgumu msimu huu chini ya Conte ambapo amefanikiwa kuanza katika michezo 16 tu msimu huu na juzi aliingia kutoka benchi na kufanikiwa kufunga goli moja katika ushindi wa goli 4-0 walioupata chelsea dhidi ya Brentford kwenye kombe la FA.

Kocha wa klabu ya West brom Tony Pilus amejitoa katika mchakato wa kumpata mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 huku ikihusishwa kuwa Ivanovic anaweza kujiunga na wababee wa Urusi timu ya Zenit St petersburg.

Akiongea na waandishi wa habari leo Jumatatu Conte anasema kuwa ' kiukweli sijaongea nae kuhusu haya maamuzi lakini tunauhakika yupo katika mazungumzo na timu mbalimbali lakini hadi sasa hivi sijui chochote ngoja tusubiri'.

Conte aliendelea kusema kuwa ' ameichezea chelsea mechi nyingi sana na ameshinda mataji mengi hapa, ana miaka 32 sasa hivi bado ana uwezo wa kucheza miaka mingi katika ligi kubwa lakini ni vizuri kuheshimu maamuzi ya mchezaji.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!