Searching...
Image and video hosting by TinyPic
13 April 2015
Monday, April 13, 2015

Tanzania kushiriki mashindano ya Kigali



Na George Mganga
Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazotegemewa kushiriki mbio za Kigali Marathon zitakazofanyika May 23-24, huku nchi kadhaa zikialikwa.
Michuano hiyo itakuwa ni ya wazi ya kimataifa, kama yalivyo ya Kilimanjaro Marathon yanayofanyika kila mwaka nchini Tanzania huku wakimbiaji kutoka nchi mbalimbali kama vile Kenya wakishiriki.
Kwa mujibu wa waandaaji, chama cha riadha nchini Rwanda (RAF), mbio hizo za Kigali pia zitakuwa na msisitizo wa kudumisha amani kupitia michezo wakimbiaji watashindana katika mbio ndefu (kilometa 42) na half marathon (kilometa 21) kwa upande wa wanawake na wanaume. Mbio hizo zitaanza uwanja wa Amahoro.
Wanariadha wengi kwa sasa wapo katika matayarisho na mashindano mbalimbali yakiwemo ya Olimpiki yatakayofanyika Rio de Janeiro, Brazil mwaka 2016.
BBC Sports

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!