Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 January 2015
Friday, January 16, 2015

Uchambuzi: Manchester City vs Arsenal


Na Chikoti Cico

Huku Aguero kule Sanchez, ndivyo unavyoweza kusema kwenye mechi itakayopigwa siku ya Jumapili kuanzia saa 1 kamili jioni katika uwanja wa Etihad pale ambapo Manchester City itakapoikaribisha timu ya Arsenal kwenye mfululizo wa mechi za ligi kuu nchini Uingereza.

Wenyeji Manchester City ambao wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi huku wakiwa na alama 47 wanatarajiwa kuingia kwenye mchezo huo kutafuta alama tatu muhimu ili kuifukuzia timu ya Chelsea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ambayo wamepishana kwa alama mbili tu.

Kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini kwenye mchezo huo atawakosa viungo Samir Nasri ambaye ni majeruhi na atakuwa nje kwa muda wiki tatu mpaka nne na Yaya Toure ambaye anaiwakilisha timu ya taifa ya Ivory Coast kwenye michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika.

Kuelekea mchezo huo takwimu zinaonyesha City hawajafungwa katika michezo 12 iliyopita ya ligi huku wakiwa wameshinda michezo tisa na kutoka sare michezo mitatu.

Kikosi cha Manchester City kinaweza kuwa hivi: Hart, Zabaleta, Demichelis, Kompany, Clichy, Milner, Silva, Navas, Fernando, Fernandinho, Aguero.

Kwa upande wa timu ya Arsenal kocha Arsene Wenger kwenye mchezo huo ataendelea kuwakosa Danny Welbeck, Jack Wilshere, Mathieu Debuchy, Mikel Arterta na Abou Diaby ambao ni majeruhi huku beki Kieran Gibbs akitarajiwa kurejea kikosini baada ya kuwa nje kwasababu ya kuwa majeruhi.

Arsenal inayoshika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 36 inatarajiwa kucheza kwa nguvu zote kwenye mchezo huo kutafuta alama tatu muhimu ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kuingia kati ya nafasi nne za juu (top four) kwenye msimamo wa ligi.

Kwa upande wa Arsenal takwimu zinaonyesha katika michezo 11 ya ugenini ndani ya msimu huu kwenye ligi wameshinda michezo minne na kufungwa michezo minne huku wakitoka sare michezo mitatu.

Pia takwimu zinaonyesha katika michezo saba iliyopita ya ligi kwenye uwanja wa Etihad kati ya Man City dhidi ya Arsenal yamefungwa magoli 24 kwa ujumla.

Kikosi cha Arsenal kinaweza kuwa hivi: Ospina, Monreal, Chambers, Koscielny, Mertesacker, Bellerin, Ramsey, Flamini, Oxlade-Chamberlain, Cazorla, Sanchez

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!