Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 January 2015
Friday, January 09, 2015

Timu zitakazo athirika kwa wachezaji wake kucheza AFCON


Na Chikoti Cico

Kuelekea michuano ya kombe la mataifa ya Afrika itakayoanza tarehe 17 ya mwezi huu wa Januari mpaka tarehe 8 ya mwezi Februari nchini Equatorial Guinea, wachezaji mbalimbali wanaocheza ligi kuu nchini Uingereza watakosekana kwa muda wiki tatu wakati michuano hiyo mikubwa barani Afrika ikiendelea.

Timu ya Manchester City itamkosa kiungo wake mahiri Yaya Toure ambaye anaiwakilisha timu ya taifa ya Ivory Coast kwenye michuano hiyo ya AFCON katika michezo mitatu dhidi ya Everton, Arsenal na Chelsea na kama Ivory Coast itasonga mbele zaidi kwenye michuano hiyo pia atakosekana dhidi ya Hull City na Stoke City.

Nae Kolo Toure ambaye ni kaka wa Yaya Toure atakosekana kwenye mechi kadha za klabu ya Liverpool dhidi ya Sunderland, Aston Villa na West Ham na pia anaweza kukosekana kwenye michezo miwili ya kombe la Capital One dhidi ya Chelsea wakati akiiwakilisha Ivory Coast.

Nayo klabu ya Everton watamkosa Christian Atsu anayeiwakilisha Ghana kwenye michuano hiyo ingawa amekuwa akitumika mara chache klabuni hapo lakini atakosa mechi dhidi ya Man City, West Brom na Crystal Palace lakini pia inawezekana akakosekana kwenye mechi dhidi ya Liverpool na Chelsea.

Nae mshambuliaji mahiri wa Swansea Wilfried Bony ambaye ataiwakilisha Ivory Coast kwenye michuano hiyo atakosekana kwenye mechi za Swansea dhidi ya West Ham, Chelsea na Southampton pia inawezekana akakosekana dhidi ya Sunderland na West Brom.

Nayo klabu ya Crystal Palace itamkosa Yannick Bolasie anayeiwakilisha Congo kwenye michuano ya AFCON na atakosekana dhidi ya Tottenham, Burnley na Everton na pia inawezekana akakosekana kwenye mchezo dhidi ya Newcastle United.

Leicester City itawakosa wachezaji wawili wa kikosi cha kwanza ambao ni Riyad Mahrez atakayeiwakilisha Algeria na Jeffrey Schlupp atakayeiwakilisha Ghana hivyo wachezaji hao watakosekana kwenye mechi dhidi ya Aston Villa, Stoke City na Manchester United lakini pia inawezekana wakakosekana dhidi ya Crystal Palace na Arsenal kama timu zao zitafika mbali kwenye michuano hiyo.

Papiss Cisse wa Senegal na Check Tiote wa Ivory Coast kwa pamoja watakosekana kwenye mechi za Newcastle United dhidi ya Southampton, Hull City na Stoke City lakini pia dhidi ya Crystal Palace kama timu mataifa hayo yatafika mbali.

Emmanuel Mayuka kutoka Senegal ambaye amekuwa akitumika kama mchezaji wa akiba kwenye klabu ya Southampton atakosekana kwenye michezo dhidi ya Manchester United, Newcastle na Swansea pia inawezekana akakosekana dhidi ya QPR na West Ham ikitegemeana na kama Senegal watafika mbali.

Mshambuliaji wa Stoke City, Mame Biram Diouf ambaye ataiwakilisha Senegal kwenye michuano hiyo ya AFCON atakosekana kwenye mechi dhidi ya Arsenal, Leicester na QPR na inawezekana pia akakosekana dhidi ya Newcastle na Man City.

Nayo timu ya Tottenham itamkosa kiungo, Nabil Bentaleb atakayeiwakilisha timu ya Algeria kwenye michuano ya AFCON na atakosekana kwenye mechi mbili za kombe la Capital One dhidi ya Sheffield United pia mechi za ligi dhidi ya Crystal Palace, Sunderland na West Brom pia anaweza akakosekana dhidi ya Arsenal na Liverpool ikitegemeana na hatua ambayo Algeria watafikia.

Kocha mpya wa West Brom Tony Pulis atamkosa Youssouf Mulumbu atakayeiwakilisha Congo kwenye michezo dhidi ya Hull City, Everton na Tottenham na pia dhidi ya Burnley na Swansea kama Congo watafika mbali kwenye michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Kwa upande wa timu ya West Ham Diafra Sakho na Cheikhou Kouyate watakoiwakilisha Senegal kwenye michuano hiyo watakosekana kwenye mechi dhidi ya Swansea, Hull City na Liverpool na inawezekana pia wakakosekana dhidi ya Manchester United na Southampton.

Ingawa mpaka sasa kuna mgogoro kati ya kocha wa West Ham na kocha wa Senegal katika swala la kumjumuisha Sakho kwenye kikosi cha Senegal huku West Ham wakisisitiza kwamba Sakho ni majeruhi hivyo hatakiwi kucheza michuano hiyo ya AFCON.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!