Searching...
Image and video hosting by TinyPic
11 January 2015
Sunday, January 11, 2015

Kina Toure wamsifia Bony.


Na Chikoti Cico

Kolo na Yaya Toure kwa pamoja wamsifia mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast na klabu ya Swansea City Wilfried Bony ambaye anahusishwa kuhamia klabu ya Manchester City kwenye dirisha hili dogo la usajili.

Wachezaji hao wote wako Abu Dhabi kwenye maandalizi ya michuano ya mataifa ya Afrika inayotarajiwa kuanza tarehe 17 ya mwezi Januari mpaka tarehe 8 ya mwezi Februari nchini Guinea ya Ikweta.

Toure akimwongelea mshambuliaji huyo alisema “ Manchester City ni klabu inayohitaji wachezaji muhimu kama Bony na Aguero, mara zote inataka kuendelea na kuwa juu kwenye ligi ya Primia”.

Kama unahitaji kuwa juu kwenye ligi ya Primia unahitaji kusaini wachezaji bora na Bony ni mmojawapo kwasasa. Itakuwa ngumu kunyakua kombe kwa mara nyingine kwasababu Chelsea wako vizuri, haijamalizika na tunahitaji kushindana vizuri na kufanya biashara tena”

Naye beki wa Liverpool Kolo Toure alimfananisha Bony na Didier Drogba kwa kusema “alianza kufunga magoli kwa haraka sana, na ndiyo maana ni kama Drogba, pia ana nguvu, mkubwa na anatumia mwili wake vizuri sana”

Wakati huo huo taarifa nchini Uingereza zinasema ofa ya kiasi cha pauni karibu milioni 30 kutoka kwa Manchester City kwaajili ya Bony imekubaliwa na Swansea hivyo mshambuliaji huyo mwenye magoli 20 katika mwaka 2014 anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne kuichezea Man City na kupokea mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!