Searching...
Image and video hosting by TinyPic
8 January 2015
Thursday, January 08, 2015

Mkombozi wa Liverpool arejea Anfield.


Na Oscar Oscar Jr

Hatimaye klabu ya Liverpool inaweza kuibuka na kufanya vizuri kufuatia kurejea kwa mshambuliaji wa timu hiyo, Daniel Sturridge. Sturridge ambaye mara ya mwisho kucheza ilikuwa ni Agosti 31 mwaka jana.

Mchezaji huyo mwenye umri wa mika 25 anatarajiwa kurejea nchini Uingereza ndani ya masaa 48 yajayo baada ya kuwa nchini Marekana kwa uangalizi na matibabu yake.

Liverpool ambayo inakamata nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza huku wakiwa wameshafunga mabao 28, hawaonekani kufanya vizuri hasa katika idara ya ushambuliaji na ulinzi.

Washambuliaji kama Fabio Borini, Mario Balotelli na Rickie Lambert, hakuna hata mmoja anayeonekana kuwa kwenye ubora wa kuisaidia Liverpool licha ya baadhi yao kupewa nafasi kiduchi kikosi cha kwanza huku kiungo, Raheem Sterling akianzishwa kama mshambuliaji wa mwisho kwenye mechi kadhaa.

Sturridge ambaye alifunga mabao 21 msimu uliopita, atakuwa fiti kabisa mwezi huu wa January ingawa kocha Brendani Rodgers amedai kuwa hawezi kuharakisha kumtumia dimbani akihofia kumletea shida mchezaji huyo. 

Sturridge ambaye ameshafunga mabao 36 kwenye michezo 52 akiwa na Liverpool, anatajwa kama mkombozi wa safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kama ambavyo aliweza kufanya vizuri msimu wake wa kwanza aliposajiliwa akitokea klabu ya Chelsea kipindi cha Januari.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!