Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 January 2015
Saturday, January 03, 2015

Mtu kachezea bao saba!
Na Florence George


Klabu ya soka ya West Brom ikiwa chini ya kocha wake mpya Tony Pulis, imefanikiwa kuivurumisha timu ya soka ya Gateshead inayoshiriki ligi daraja la tano nchini Uingereza magoli 7-0 katika mchezo wa kombe la FA uliochezwa siku ya jumamosi katika dimba la Hawthorns.

  
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa kwanza kwa kocha, Tony Pulis ambaye alichukua nafasi hiyo baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Alan Irvine kutimuliwa mwishoni mwa mwezi December baada ya mwenendo mbaya wa timu hiyo katika ligi kuu nchini humo.

Gateshead walikuwa hawajaruhusu kufungwa goli katika michezo waliyokuwa wamecheza katika kombe la FA klaba ya kukumbana na kipigo hicho kutoka kwa West Brom.


Mchezaji wa kimataifa wa Uingereza mwenye asili ya Burundi, Saido Berahino alifanikwa kufunga magoli manne peke yake na kutimiza idadi ya magoli 13 ambayo tayari ameshafunga msimu huu.

Mchezo huo kwa asilimia kubwa ulitawaliwa na wenyeji huku Anichebe ,Brunt na Morrison kila mmoja akifunga goli moja na kuisaidia West Brom kutinga katika hatua ya nne ya kombe hilo.


Mara baada ya mchezo huo kocha Pulis alisema kuwa Berahino ni mchezaji mwenye kipaji na uwezo mkubwa wa kucheza mpira na anaamini ataweza kufanya nae kazi kwa muda mrefu katika timu hiyo.

Katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza West Brom wanashika nafasi ya 17 huku wakiwa na pointi 18 pointi moja zaidi ya Crystal Palace na Burnley zenye pointi 17 katika michezo 20 waliyocheza mpaka sasa.  


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!