Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 January 2015
Saturday, January 03, 2015

Atletico yashinda huku Torres akiwa Jukwaani.


Na Oscar Oscar Jr

Bingwa mtetezi wa ligi kuu nchini Hispania, klabu ya Atletico Madrid imerejea kwa kishindo baada ya ligi hiyo kusimama kwa muda kwa kupata ushindi wake mnono wa mabao 3-1 dhidi ya timu ya Levente huku mshambuliaji Fernando Torres akishuhudia mchezo huo akiwa kwenye jukwaa.

Magoli ya Atletico Madrid yalifungwa na Antoine Griezmann ambaye alifunga mabao mawili huku Diego Godin akitupia bao moja na lile la kufutia machozi kwa upande wa Levante liliwekwa wavuni na El Zhar. 

Ushindi huo umewafanya vijana hao wa kocha Diego Semeone wafungane kwa pointi na Barcelona (38) ambao kesho nao watashuka dimbani huku wakizidiwa alama moja tu na vinara Real Madrid ambao wamecheza michezo miwili pungufu.

Torres hakuweza kuruhusiwa kucheza mchezo huo kwa sababu uhamisho wake bado haujakamilika na hii inatokana na dirisha la usajili nchini Italia kufunguliwa rasmi siku ya Jumatatu hivyo, hatoweza kucheza mchezo wowote hadi siku ya Jumatatu ambapo taratibu zote zitakuwa zinakamilishwa.

Semeone ameamua kuongeza nguvu kwenye safu yake ya ushambuliaji ambayo mpaka sasa imefunga mabao 34 huku Barcelona wakiwa na magoli 41 na Real Madrid ndiyo vinara wa kila kitu kwani wameshafunga mabao 45 kwenye michezo 15 tu.

Ujio wa Fernando Torres atakuja kutengeneza ushirikiano na washambuliaji kama  Antoine Griezmann na Mario Mandzukic ambaye alisajiliwa msimu huu akitokea klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani.

Mpaka sasa Griezmannn ndiye mfungaji bora wa Atletico Madrid akiwa na mabao nane akifuatiwa na Mario Mandzukic ambaye ameshafunga mabao sita. 

Torres baada ya kutoka Liverpool ameshindwa kuonyesha makali yake akiwa na Chelsea na baadaye Ac Millan na hii ni nafasi ya pekee kuweza kurejesha makali yake.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!