Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 January 2015
Saturday, January 03, 2015

Kagera Sugar yazifikia Yanga na Azam fc.


Na Oscar Oscar Jr

Kagera Sugar ambao walikuwa ugenini leo hii kwenye uwanja wa Mabatini, wameweza kutoshana nguvu na Ruvu Shooting kwa kutoka sare pacha huku timu zote zikionyesha mchezo mzuri. 

Kwa upande wa Ruvu Shooting, wao wamepeleka lawaza zao kwa mwamuzi wa mchezo huo na kudai kuwa walistahili kupata penalty kupitia msemaji wa klabu hiyo, Masau Bwire.

Kagera ambao mechi iliyopita walitoka kuwalaza wekundi wa Msimbazi timu ya Simba kwa bao 1-0, matokeo hayo yanawafanya kuweza kutimiza alama 14 na sasa kuwa sawa kwa pointi na timu za Yanga na Azam licha ya wanankurunkumbi hao kuwa mbele kwa mchezo mmoja.

Ruvu Shooting ambao mechi iliyopita walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu JKT, sasa wametimiza alama 11 na mchezo unaofuata watasafiri hadi Tanga kwenda kucheza na timu ya Mgambo JKT kabla ya kwenda Dar es Salaam kuvaana na timu ya Yanga kwenye mzunguko wa 11.

Kwa upande wa Kagera Sugar, wao watarejea sasa nyumbani kuwasubiri mabingwa watetezi timu ya Azam kwenye dimba la Kaitaba na kwenye mzunguko wa 11, watasalia ndani ya Kaitaba kuwaalika Mbeya City kutoka Jijini Mbeya.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!