Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 January 2015
Friday, January 09, 2015

Chelsea na dirisha la usajili.


Na Oscar Oscar Jr

Vinara wa ligi kuu ya Uingereza, Chelsea wanajiandaa kushindana ili kuweza kumnasa kiungo mshambuliaji wa Borussian Dortmund, Marco Reus huku pia wakimsaka beki wa kati wa Real Madrid, Mfaransa Raphael Varane. 

Imekuwa muda sasa kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amekuwa na nia ya kutafuta mbadala wa John Terry na sasa ameanza kumsaka Varane.

Katika klabu ya Chelsea kumekuwa pia na habari za kutaka kuondoka kwa kipa Peter Cech huku Arsenal ikiwa ni moja ya klabu zinazomuhitaji mlinda mlango huyo. 

Chelsea wamegoma kumuuza mchezaji huyo katika dirisha hili huku hali ikionyesha kuwa, baada ya kumalizika kwa msimu huu mchezaji huyo ataruhusiwa kuondoak kwenye klabu hiyo.

Kiungo mshambuliaji wa Ujerumani, Andre Schurrle ametajwa kutakiwa na klabu ya Bundesliga, Wolfsburg ambao tayari wametoa Pauni 23M kwa ajili ya mchezaji huyo. 

Wolfsburg ambao wanakamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Ujerumani, wanataka kuongeza nguvu ili kuweza kupambana na Bayern Munich ambao wanaonekana kutopoteza mchezo wowote mpaka sasa.

Wiki hii kumekuwa na habari kubwa ya Lionel Messi kutaka kuondoka kwenye klabu ya Barcelona huku klabu za Chelsea na Manchester City zikitajwa kumuhitaji mchezaji huyo.

Kwa taarifa zilizotoka leo, zinaeleza kuwa Lionel Messi atakuwa tayari kuondoka Barcelona endapo itapatikana timu ambayo itampatia Pauni 500M.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!