Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 December 2014
Saturday, December 20, 2014

Yanga vs Stand United Desemba 24 pale Taifa.


Na Oscar Oscar Jr

Baada ya aliyekuwa kocha wa timu ya Yanga, Marcio Maximo mkataba wake kukatishwa kocha Hans Van der Pluijm anatarajia kuanza kibarua chake kwa mechi ya kirafiki iliyopangwa kuchezwa Desemba 24 dhidi ya timu ya ligi kuu Tanzania bara, Stand United.

Mara ya mwisho wakati timu hizo zimekutana kwenye mchezo wa ligi kuu kule mkoani Shinyanga, Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 huku Jerryson Tegete na mbrazil Jaja wakiwa wafungaji wa mabao hayo.

Hans Van Der Pluijm aliwahi kuiongoza Yanga msimu uliopita na kuisaidia kumaliza kwenye nafasi ya pili huku wakivuka pia mzunguko wa kwanza kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika. 

Tayari wachezaji kama Danny Mrwanda na Amis Tambwe wamesajiliwa kwenye kikosi cha Yanga na mechi hiyo inaweza kutumika kuonyesha uwezo kwa kocha huyo ambaye anakumbukwa na wana Jangwani hao kwa mchezo wake wa kuvutia.

Stand United nao wamefanya usajili wa wachezaji saba ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chao ambacho baada ya mechi saba za ligi kuu, wamejikuta wakiambulia pointi tisa na kusalia kwenye nafasi ya 10. Bado wanahitaji kuongeza nguvu hasa katika safu ya ushambuliaji ambapo mpaka sasa wamefunga mabao matano pekee.

Ligi kuu inatarajiwa kuendelea tena Desemba 26 kwa mchezo mmoja tu ambapo Simba watawakaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa huku, Stand United wakisafiri hadi Morogoro Desemba 27 kwenda kupambana na vinara wa ligi hiyo timu ya Mtibwa Sugar. 

Kwa upande wa pili, Yanga watakuwa wakishuka dimbani Desemba 28 kumenyana na mabingwa watetezi wa ligi hiyo, timu ya Azam ambao wamekwenda kuweka kambi nchini Uganda.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!