Searching...
Image and video hosting by TinyPic
22 December 2014
Monday, December 22, 2014

Waamuzi wanaotambuliwa na FIFA kutoka Tanzania



Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limetoa orodha mpya ya waamuzi linaowatambua ,Kwenye orodha hiyo kuna jumla ya waamuzi 18 kutoka Tanzania,miongoni mwa waamuzi hao waamuzi 11 wapya na 7 wa zamani.

Waamuzi wapya wa kati kutoka Tanzania ni Mfaume Ali Nassor kutoka visiwani Zanzibar pamoja na Martin Saanya kutoka Morogoro, pia wamo waamuzi watatu wa kike ambao ni Florentina Zabron ,Jonesia Rukyaa pamoja na Sofia Ismail.

Kwa upande wa waamuzi wasaidizi wanaume ni Frank John Komba na Soud Idd Lila , kwa upande wa wanawake ni Kudura Omary Maurice,Hellen Joseph Mduma,Dalila Jafari Mtwana na Grace Mawala.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa website ya bbc swahili.

Waamuzi wa zamani wa Tanzania kwenye orodha ya FIFA ,kwa upande wa wanaume ni Israel Mujuni Nkongo na Waziri Sheha Waziri,kwa upande wa waamuzi wasaidizi ni Josephat Bulali,Fernand Chacha,John Longino Kanyenye ,Ali Kinduli na Samuel Hudson Mpenzu .

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!