Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 December 2014
Sunday, December 28, 2014

Uchambuzi: Mbeya City vs Ndanda Fc


Na Oscar Oscar Jr

Katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya leo utapigwa mchezo kati ya Mbeya City dhidi ya Ndanda Fc kutoka mkoani Mtwara. Ndanda Fc ndiyo timu iliyoruhusu kufungwa magoli mengi msimu huu (12) huku nusu ya magoli hayo yakifungwa kwa mipira ya adhabu.

Mbeya City ambao wanakamata nafasi ya mwisho (14) kwenye ligi kuu huku wakiwa na alama tano, watakuwa na kibarua cha kurejesha imani kwa wananchi wa Mbeya ambao wameonekana kuanza kuikatia tamaa timu hiyo ambayo mpaka sasa imeshinda mechi moja tu, kutoka sare mara mbili na kupoteza mechi nne.

Mbeya City ambao wamewaondoka kikosini baadhi ya wachezaji walioing'arisha timu hiyo msimu uliopita kama mshambuliaji Saad Kipanga na kiungo Anthony Matogolo, watavaana na Ndanda Fc ambayo pamoja na kuchechemea wakiwa kwenye nafasi ya 13, walifanikiwa kumfunga bingwa mtetezi timu ya Azam kwa bao 1-0.

Tatizo kubwa la Mbeya City limekuwa kwenye safu ya ushambuliaji ambapo mpaka sasa wamefunga mabao mawili tu yaliyopatikana kwa njia ya peneti. Ndanda pamoja na kuruhusu mabao mengi, bado wamefanikiwa kufunga mabao saba.

Mchezo huu utakuwa na presha kubwa kwa Mbeya City na matokeo tofauti na ushindi, yanaweza kusababisha hali ya sintofahamu ndani ya timu hiyo inayomilikiwa na Halmashauri ya jiji. 

Mbeya City wanahitaji pointi tatu kwenye mchezo wa leo ili waweze kujiandaa vema kwenye mchezo unaofuata ambapo watashuka dimbani Sokoine kucheza na timu ya Yanga Desemba, 03, 2015.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!