Searching...
Image and video hosting by TinyPic
22 December 2014
Monday, December 22, 2014

Vita ya Carlos Tevez vs Gonzalo Higuain kule Doha-Qatar


 Na Oscar Oscar Jr

Baada ya kushinda mara mbili mfululizo Italian Super Cup, Juventus wamejikuta wakiangukia pua baada ya kutandikwa na Napoli kwenye mchezo wa fainali uliopigwa huko Doha nchini Qatar na kushuhudia timu hizo zikicheza kwa dakika 120 huku matokeo yakisalia kuwa mabao 2-2.

Juventus ambao wamekuwa wafalme kwenye soka la Italia kwa misimu ya hivi karibuni, walikuwa wanaongoza mara zote kupitia magoli ya mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina, Carlos Tevez lakini Muargentina mwingine wa Napoli, Gonzalo Higuain alikuwa anasawazisha mambo na baadaye, mikwaju ya penati ikatumika kuamua bingwa.

Akizungumza baada ya ushindi huo kocha wa Napoli, Muhispania Rafael Benitez amesema kuwa, ushindi huo ni moja kati ya vitu ambavyo hatokuja kuvisahau katika maisha yake.

Carlos Tevez alifunga bao dakika ya tano tu ya mchezo huku Higuain akisawazisha mnamo dakika ya 68 na dakika disini zikamalizika kwa sare ya 1-1

Baada ya kuongezwa dakika nyingine 30, ndipo Tevez aliweza tena kuipatia Juventus bao la kuongoza na la pili kwake dakika116 lakini baadaye, Higuain akasawazisha tena dakika ya 118 na kuupeleka mchezo kwenye matuta ambako Napoli wameshinda kwa penati 6-5.

Juventus bado wanaongoza kwenye mbio za kuwania kutetea kwa mara nyingine tena ubingwa wa Seria A wakiwa na alama 39, As Roma wakiwa nafasi ya pili na alama 36 huku Napoli wao, wanashika nafasi ya tatu wakiwa na alama 27 kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Italia.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!