Searching...
Image and video hosting by TinyPic
6 November 2014
Thursday, November 06, 2014

Stand United vs Mbeya City Jumamosi hii-Kambarage Shinyanga.


Na Oscar Oscar Jr

Unapotazama msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya mechi sita kupigwa, unakutana na timu ya Mbeya City ikiwa kwenye nafasi ya mwisho (14). 

Ukitazama nafasi mbili za juu, unakutana na majina ya Mtibwa Sugar na Coastal Union. Simba, Yanga na Azam wako wanajikongoja, hii ni ishara tosha kuwa ligi imeongeza ushindani.

Jumamosi hii kwenye uwanja wa Kambarage pale mkoani Shinyanga, utapigwa mchezo wa ligi kuu kati ya Stand United dhidi ya Mbeya City. 

Stand United wameshuka dimbani kwenye uwanja wa nyumbani mara tatu lakini, bado hawashinda mchezo wowote. Walifungwa na timu za Ndanda Fc na Yanga huku wakitoka sare na Tanzania Prisons juma lililopita.

Stand United wanahitaji kupata ushindi wa pili kwenye ligi na wa kwanza wakiwa mbele ya mashabiki wao ambao kila weekend hujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono. 

Hii itakuwa ni mechi ngumu kwa sababu, Mbeya City nao baada ya kuwa na mwanzo mbaya, wanahitaji matokeo ya ushindi ili waweze kurejesha imani kwa wapenzi wao na wadau wa soka nchini ambao wanaonekana kuanza kuwakatia tamaa.

Msimu uliopita baada ya mechi sita za awali, Mbeya City walikuwa hawajapoteza mchezo hata mmoja. Walikuwa wameshinda mara moja na kutoka sare mara tano huku ratiba ikiwakutanisha na timu za Simba na Yanga. 

Mambo sio mazuri kwa upande wao hususani kwenye safu yao ya ushambuliaji ambayo mpaka sasa, imefunga mabao mawili pekee.

Stand United wako kwenye nafasi ya 13 baada ya kujikusanyia alama sita huku Mbeya City, wakiwa wa 14 huku wakiwa na alama tano pekee. Ushindi kwa Mbeya City unaweza kuwavusha mpaka nafasi ya saba huku ushindi kwa Stand United, unaweza kuwafikisha nafasi ya sita.

Ligi bado ni ngumu kwa sababu, timu inaposhinda michezo miwili mfululizo, inapata nafasi ya kuwekwa kwenye timu zinazopigania ubingwa huku vichapo mara tatu mfululizo, vinaweza kukupeleka kwenye timu zinazohisiwa kushuka daraja.

Matokeo ya Stand United mpaka sasa.

Stand United 1-4 Ndanda Fc
Mgambo JKT 0-1 Stand United
Simba 1-1 Stand United
Kagera Sugar 0-0 Stand United
Stand United 0-3 Yanga
Stand United 1-1 Tanzania Prisons

Matokeo ya Mbeya City mpaka sasa.

Mbeya City 0-0 Ruvu JKT
Mbeya City 1-0 Coastal Union
Ruvu Shooting 0-0 Mbeya City
Mbeya City 0-1 Azam Fc
Mbeya City 0-2 Mtibwa Sugar
Mgambo JKT 2-1 Mbeya City



0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!