Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 November 2014
Sunday, November 09, 2014

Simba kibaruani leo Taifa.


Na Oscar Oscar Jr

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara, timu Azam jana waliweza kujipatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union kutoka mkoa wa Tanga mchezo uliopigwa kwenye dimba la Azam Complex, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Matokeo hayo yanaendelea kuwabakiza kwenye nafasi ya tatu baada ya kutimiza pointi 13. Mabingwa mara 24 wa ligi kuu Tanzania bara, timu ya Yanga nao jana walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam dhidi ya Mgambo JKT. Ushindi huo unawafanya Yanga nao kutimiza alama 13 wakiwa nafasi ya pili na tofauti ya magoli pekee ndiyo inawatengenisha na Azam.

Kwa upande wa Mbeya City, wao mambo hayakuwa mazuri baada ya kujikuta wakichezea kichapo cha nne mfululizo msimu huu pale walipofungwa bao 1-0 na timu ya Stand United mchezo uliofanyika kwenye dimba la Kambarage mkoani Shinyanga. 

Matokeo hayo yanaendelea kuwaacha Mbeya City mkiani mwa msimamo wa ligi kuu na alama zao tano huku, Stand United wao wakitimiza alama tisa na kujinasua kutoka kwenye timu tatu za chini.

Mchezo mwingine ulipigwa kule kwenye dimba la Jamhuri mkoani Morogoro ambapo, timu ya Polis Morogoro ilikuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons na mwisho wa mchezo, Polis Moro waliweza kuibuka na pointi zote tatu baada ya kuwafungwa Prisons bao 1-0.

Nako mkoani Morogoro kulikuwa na mchezo mwingine kati ya vinara wa ligi kuu, timu ya Mtibwa Sugar ambao walicheza dhidi ya Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera na mpambano huo Uliahirishwa kufuatia hali ya hewa ambayo haikuwa rafiki kwa mchezo wa soka. 

Matokeo yaliyotufikia baada ya mchezo huo kupigwa asubuhi ya leo, timu hizo zimetoshana nguvu na kwenda sare ya 1-1. Kwa matokeo hayo, Mtibwa Sugar wanaendelea kukaa kileleni baada ya kufikisha alama 15 na tofauti yao na timu za Yanga na Azam, inaendelea kuwa ni pointi mbili pekee.

Michezo mingine miwili inatarajiwa kupigwa leo kwenye viwanja viwili tofauti ambapo Simba watakuwa uwanja wa Taifa kuwa karibisha Ruvu Stars kutoka mkoa wa Pwani huku, katika dimba la Chamazi ukipigwa mchezo kati ya maafande wa Ruvu JKT ambao watapambana na timu ya Ndanda kutoka mkoa wa Mtwara.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!