Searching...
Image and video hosting by TinyPic
10 November 2014
Monday, November 10, 2014

Jamie Carragher aichana laivu Arsenal


Na Chikoti Cico

Beki wa zamani wa Liverpool na timu ya taifa ya Uingereza, Jamie Carragher aichambua Arsenal kwa kuonyesha mchezo mbovu dhidi ya Swansea.

Carragher ambaye kwasasa ni mchambuzi wa soka aliongea hayo akiwa kwenye studio za Sky Sports 1 baada ya mechi ya Swansea City dhidi ya Arsenal mchezo ulioisha kwa Swansea kushinda kwa magoli 2-1.

Akiongelea mbinu za kocha wa Arsenal, Carragher alisema “Nimesema mara milioni katika miezi 12 iliyopita, kitu hichohicho na hakuna jipya.

"Kabla ya mchezo Wenger alikuwa anacheka sifikiri kama atakuwa anacheka sasa, alisema (Wenger) anapata uwiano sawa kati ya kushambulia na kuzuia. Kwa goli la kusawazisha (la Swansea) alikuwa na wachezaji saba ama nane mbele ya mpira zikiwa zimebaki dakika 15”

Aliendela kusema “kivipi unashambuliwa kwa mipira ya kushtukiza (counter attack) wakati unaongoza goli moja na zikiwa zimebaki dakika 15 mpira kuisha, nafasi moja Swansea waliyoonyesha ubora kwenye eneo la 18 Monreal alipitwa kama wote tulivyojua angepitwa tu”

Carragher aliyestahafu soka mwishoni mwa msimu wa 2012/2013 akiongelea kuhusu Wenger kushindwa kufanya usajili wenye tija kwa timu yake akifananisha na Chelsea alisema “Chelsea na Arsenal wanaoneakana wana umbali tofauti na hiyo ni kwasababu Mourinho aligundua anachohitaji, timu yake Mourinho inaonekana haikamatiki na hayo ni matokeo ya usajili huo”

Carragher akiendela kuuchambua usajili wa Arsenal alisema “Walimwacha Vermaelen aondoke na hawakupata mbadala, vitu vidogo hivi ndivyo huigharimu Arsenal ikiwa juu (kwenye msimamo wa ligi)

Ingawa Wenger ameweza kuwasajili Alexis Sanchez, Danny Welbeck, Calum Chambers na Mathieu Debuchy, lakini bado Carragher anahisi usajili huo hautoshi kuifanya Arsenal iwe bora.

Carragher alimalizia kwa kusema “Walikuwa na msimu mzuri zaidi ya Chelsea lakini kwasasa wanajiskia wako mbali nao, Mourinho aliona maeneo yaliyohitajika kuboreshwa na akasajili kwenye maeneo hayo, Ila kutokea msimu uliopita (Arsenal) walionekana kama wamerudi nyuma”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!