Searching...
Image and video hosting by TinyPic
15 October 2014
Wednesday, October 15, 2014

Uchambuzi : Polisi Moro vs Mtibwa Sugar


Na Oscar Oscar Jr

Katika dimba la Jamhuri pale mkoani Morogoro jumamosi hii kutakuwa na mechi dhidi ya timu mbili zinazotoka katika mkoa huo, Polis Moro dhidi ya Mtibwa Sugar. 

Mtibwa Sugar wanaongoza ligi kuu Tanzania bara wakiwa na alama tisa baada ya kushinda michezo yao yote mitatu ya awali huku Polis, wakishika nafasi ya 11 baada ya kupoteza mchezo mmoja na kutoka sare mara mbili.

Polis Moro ni timu ambaye imekuwa na utamaduni wa kupanda daraja na kushuka na kama wanataka kuepuka dhahama hiyo, wanatakiwa kuanza kupata ushindi kuanzia kwenye mchezo huu ambao wao ndiyo wenyeji. 

Mtibwa wanaonekana kudhamiria kufanya vizuri msimu huu na kurejesha heshima yao na huu utakuwa ni mfupa mgumu kwa Polis Moro.

Timu hizi mara ya mwisho kukutana kwenye ligi kuu ilikuwa msimu wa 2012/2013 na michezo yote miwili, Mtibwa hakufurukuta. Mechi ya kwanza ilimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 huku mechi ya marudiano, Mtibwa alilazwa bao 1-0.

Timu ya Polis Moro ina mchanganyiko wa wachezaji vijana na wakongwe kwenye idara zote na hicho ndicho kinachowapa balance ya timu. 

Wozoefu kama Salumu Machaku na Dany Mrwanda wameonekana kuifanya timu hiyo kuwa imara sana kwa mechi zao za awali hasa kwenye mechi zao dhidi ya Simba na ile ya Kagera Sugar.

Mechi tatu za Polis Moro msimu huu.

Azam 3-1 Polis Moro
Simba 1-1 Polis Moro
Polis Moro 1-1 Kagera Sugar

Mechi tatu za Mtibwa msimu huu.

Mtibwa Sugar 2-0 Yanga
Mtibwa Sugar 3-1 Ndanda fc
Mtibwa Sugar 1-0 Mgambo JKT

Mchezaji wa kuchungwa kwa Mtibwa Sugar.

Ally Shomary ndiye mfungaji bora wa Mtibwa Sugar mpaka sasa ameshafunga magoli matatu. Safu ya ulinzi ya Polis Moro imtazame mshambuliaji huu kwa jicho la tatu na kupunguza makosa ya kizembe kama walivyofanya dhidi ya Kagera Sugar. 

Ally Shomary anashika nafasi ya pili katika ufungaji bora kwenye ligi kuu bara akiwa nyuma ya Didier Kavumbagu wa Azam ambaye amefunga jumla ya mabao manne.

Mchezaji wa kuchungwa kwa Polis Moro.

Pamoja na kuwa umri umekwenda, Danny Mrwanda bado anaonekana ni moja ya washambuliaji wasumbufu sana. Anajua namna ya kulisaka bao na anapopata nafasi huitumia vema. 

Alifanya hivyo kwenye mechi yao dhidi ya Simba na kupachika bao na ni moja kati ya watu wa kuwatazama kwenye mechi yao dhidi ya Mtibwa Sugar.

Polis Moro tayari wameruhusu kufungwa magoli matano mpaka sasa na hii imechangawi na makosa binafsi ya walinzi wake wa kati na kukosa mawasiliano mazuri na mlinda mlango wao. 

Wanaenda kucheza na Mtibwa Sugar ambako yuko Mussa Hassan Mgosi na Ame Ally, ni lazima polis waimarike ili kuweza kukabiliana na nguvu ya washambuliaji hao.

Mtibwa ni timu inayobadilika kulingana na aina ya mpinzania wanaye kabiliana naye. Walicheza kwa mbinu ya kubaki Bus dhidi ya Yanga na kufanya mashambulizi ya kushitukiza na wakafanikiwa kupata ushindi. 

Walipocheza dhidi ya Ndanda na Mgambo JKT, walichezo mchezo wa wazi na wakashinda mechi zote. Kwa namna Polis Moro wanavyocheza, natarajia soka la wazi kwa pande zote mbili.












0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!