Searching...
Image and video hosting by TinyPic
17 October 2014
Friday, October 17, 2014

Uchambuzi: Manchester City vs Tottenham


Na Chikoti Cico.

Baada ya kusimama kwa wiki moja kupisha michezo ya kimataifa hatimaye ligi kuu ya Uingereza maarufu kama “Barclays Premier League” imerejea tena na moja ya mechi kali za mwisho wa juma ni kati ya Manchester City dhidi ya Tottenham Hotspur, mechi itakayopigwa kwenye uwanja wa Etihad nyumbani kwa Machester city.

Wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuifunga Spurs msimu uliopita kwa magoli 6-0 nyumbani Etihad na magoli 5-1 kwenye uwanja wa White Hart Lane, timu ya Machester City wanahitaji kushinda mechi hii ili kupunguza “gap” la alama tano dhidi ya vinara wa ligi hiyo Chelsea.

Manchester City wanaoishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, wanategemea kumkosa beki wao Eliaquim Mangala aliye majeruhi pamoja na Samiri Nasri huku Yaya Toure, akitarajia kuanza kwenye mechi hiyo pamoja na kuwa alienda kuitumikia Ivory Coast kwenye mechi ya kufuzu michauano ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Kongo.

Washambuliaji wa Manchester City Edin Dzeko na Sergio Aguero wamekuwa na rekodi nzuri ya magoli dhidi ya Spurs. Takwimu zinasema mpaka sasa, Dzeko amefunga magoli sita kati ya mechi saba dhidi ya Spurs huku Aguero akifunga magoli matano kati ya mechi tano dhidi ya Spurs.

City ambao mpaka sasa wamekuwa na rekodi nzuri ugenini kuliko nyumbani tofauti na msimu uliopita kwani mpaka sasa kati ya mechi tatu nyumbani wameshinda mmoja, wamepoteza moja na kutoka sare moja huku wakishinda mechi zote nne za ugenini.

Tottenham wanaoshika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi na kama wakishinda, wanaweza kupanda mpaka nafasi ya pili ama ya tatu hivyo kocha wa Spurs Mauricho Pochettino, anatarjiwa kuingia kwenye mechi hii kwa azma ya kushinda ili kujiweka kwenye nafasi nzuri.

Spurs wataendelea kuwakosa mabeki Kyle Walker na Kyle Naughton ambao ni majeruhi huku kocha Pochettino akitaka kufuta rekodi mbaya ya mechi za ugenini hasa ikizingatiwa kati ya mechi saba za ligi mpaka sasa Spurs, wamepoteza mechi zote tatu za ugenini.

Takwimu zinasema kati ya Agasti 2011-Januari 2014 Manchester city wamekutana mara sita na Spurs kwenye ligi kuu ya Uingereza huku City wakishinda mechi 5 kati ya hizo na Spurs kushinda mechi moja huku vijana wa Pellegrini wakifunga jumla ya magoli 22 kati ya 30 kwenye mechi zote sita.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!