Searching...
Image and video hosting by TinyPic
22 October 2014
Wednesday, October 22, 2014

Uchambuzi: Liverpool vs Real Madrid



Na Chikoti Cico

Mechi kubwa iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kati ya Liverpool dhidi ya Real Madrid inatarajiwa kupigwa leo siku majira ya saa 3:45 kwa saa za Afrika Mashiriki huku wachambuzi na mashabiki mbalimbali wa soka wakiipa nafasi timu ya Real Madrid kuibuka kidedea kwenye mchezo huo.
Timu ya Liverpool inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi B ikiwa na alama tatu baada ya kushinda mchezo wa kwanza dhidi ya Ludogorets kwa magoli 2-1 na kupoteza mchezo wa pili dhidi ya Basley kwa kufungwa kwa goli 1-0 inaingia kwenye mechi ya leo ikihitaji kuibuka na ushindi ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kuvuka kwa hatua ya makundi.
Kocha Brendan Rodgers bado ataendelea kumkosa mshambuliaji Mwingereza Daniel Sturridge aliyeko majeruhi hivyo Mario Balotelli anatarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Liverpool ingawa mpaka sasa amefunga goli moja kati ya mechi tisa alizoichezea Liverpool.
Liverpool watakuwa na kazi ya kumchunga mshambuliaji wa Real Madrid Christiano Ronaldo ambaye mpaka sasa ameshafunga magoli 19 kati ya michezo 12 aliyocheza msimu huu zaidi ya timu nzima ya Liverpool ambayo kwa ujumla wamefunga magoli 14 kati ya michezo 10.
Takwimu zinaonyesha Liverpool imepoteza mechi moja tu kati ya michezo 18 iliyopita ya mashindano ya Ulaya hii ikijumuisha mechi za ligi ya Mabingwa wa Ulaya na Europa, pia kati ya mechi 14 ambazo Liverpool imekutana na timu kutoka Hispania imeshinda michezo mine, imetoka sare michezo sita na kupoteza michezo minne.
Kikosi cha Liverpool kinachoweza kuanza ni: Mignolet; Johnson, Skrtel, Lovren, Enrique; Allen, Henderson, Gerrard; Sterling, Balotelli, Lallana
Timu ya Real Madrid inayoongoza kwenye msimamo wa kundi B ikiwa na alama sita baada ya kushinda michezo yake miwili ya awali dhidi ya Basel na Ludogorets inatarajiwa kuingia kwenye mchezo wa leo wakiwa na ari ya kutafuta alama tatu muhimu ili kujihakikishia nafasi ya kuvuka hatua ya makundi na kuendelea kuongoza kundi B.
Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti ataingia kwenye mchezo huo bila ya kiungo mwenye kasi Gareth Bale ambaye ni majeruhi hivyo Ancelotti anaweza kumwanzisha kiungo wa Kihispania Isco kwenye safu ya kiungo ya Real Madrid.
Kikosi cha Real Madrid kinachoweza kuanza ni: Casillas; Carvajal, Ramos, Pepe, Marcelo; Modric, Kroos, Isco; James, Benzema, Ronaldo

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!