Searching...
Image and video hosting by TinyPic
22 October 2014
Wednesday, October 22, 2014

Uchambuzi: Anderlecht vs. Arsenal



Na Chikoti Cico


Ligi ya mabingwa ulaya iliyoshika kasi toka Jumanne ya wiki hii itaendela tena kwa mechi kati ya Anderlecht dhidi ya Arsenal moja kati ya mechi za kundi D itakayopigwa jijini Brussels Ubelgiji kwenye uwanja wa Constant Vanden Stock.

Anderlecht ambayo inashika mkia kwenye msimamo wa kundi D huku ikiwa na alama moja baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Dortmund kwa kufungwa magoli 3-0 na kutoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Galatasaray inahitajika kushinda mchezo wake dhidi ya Arsenal ili kuamsha matumaini ya kuweza kuvuka hatua ya makundi.

Kocha wa Anderlecht Besnik Hasi anatarajiwa kumkosa kiungo wa kifaransa Fabrice N’sakala ambaye aliumia goti akiwa mazoezini mwanzoni mwa mwezi wa tisa huku taarifa zikisema atakuwa nje kwa muda wa miezi miwili, huku mlinzi Bram Nuytinck ambaye alipata majeraha ya kidole cha mguu akiwa ana hati hati ya kuanza kwenye mchezo hiyo.

Takwimu zinaonyesha Anderlecht wanarekodi mbaya dhidi ya timu za Uingereza kwani katika michezo 28 waliyocheza dhidi ya timu kutoka Uingereza wameshinda michezo sita, wametoka sare michezo minne na kupoteza michezo 18.

Kikosi cha Anderlecht kinachotarajiwa kuanza ni: Proto; Vanden Borre, Mbemba, Heylen, Deschacht; Defour, Tielemans; Najar, Praet, Suarez; Mitrovic.

Timu ya Arsenal inayosumbuliwa na wachezaji wengi walioko majeruhi inatarajiwa kuwakosa Mesut Ozil , Sanogo, Debuchy, Ospina na Koscielny kwa kuumia kwa kipa Ospina huku kipa Wojciech Szczesny akiendelea kutumikia adhabu baada ya kupewa kadi nyekundu kwenye mechi iliyopita dhidi ya Galatasaray kipa namba tatu Emiliano Martinez ndiye anayetarajiwa kusimama kwenye lango la Arsenal.

Arsenal inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi D ikiwa na alama tatu baada ya kushinda mchezo uliopita dhidi ya Galatasaray kwa magoli 4-1 inatarajiwa kumwanzisha kiungo Aaron Ramsey ambaye alikuwa majeruhi hivyo kuiongezea makali safu ya kiungo ya Arsenal katika kutafuta alama tatu muhimu kwenye kundi hilo.

Kikosi cha Arsenal kinachoweza kuanza ni: Martinez; Monreal, Mertesacker, Chambers, Gibbs; Flamini, Ramsey, Wilshere; Sanchez, Cazorla; Welbeck

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!