Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 September 2014
Tuesday, September 09, 2014

England na Hispania mambo safi Euro



 Na Oscar Oscar Jr

Hatimaye "Pepo mchafu" aliyekuwa amewaandama Mabingwa wa Ulaya, timu ya taifa ya Hispania, ameanza kuondoka baada ya kupata ushindi wao wa kwanza katika hatua ya makundi ya kutafuta nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya mwaka 2016.

Hispania ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo, wamejikuta katika hali ya sintofahamu kwa sababu ya kushindwa kutamba kwenye michuano ya kombe la dunia iliyomalizika huko nchini Brazil mwaka huu kutokana na sababu mbalimbali huku kupungua kiwango kwa baadhi ya wachezaji wake muhimu ikionekana kama sababu kubwa.

Hispania wameichapa Macedonia mabao 5-1 huku mshambuliaji chipukizi Paco Alcacer aliyekuwa anachezea taifa lake katika mechi rasmi kwa mara ya kwanza, alifungua orodha ya mabao kabla ya penalty ya Sergio Ramos kuwaongezea la pili dakika za mapema jijini Valencia. 

Sergio Busquets alipachika la tatu wavuni kutoa tashwishi yeyote juu ya matokeo na goli lake la kwanza katika mechi 70 muda mfupi kabla ya mapumziko kabla ya David Silva na Pedro Rodriguez kutia kimyani katika awamu ya pili. 


Naye mshambuliaji mpya wa Arsenal, Danny Welbeck, alizamisha magoli yote mawili na kuwezesha Uingereza kujipatia ushindi wa 2-0 ugenini na kuzindua kampeni yao ya kufuzu Kombe la Ulaya la 2016 kwa msisimko mkubwa. 

Mechi hiyo iliyochezwa Basel ilishuhudia Uingereza ambao wametoka "kupewa vidonge" na vyombo vyao vya habari baada ya kucheza mchezo mbovu kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Norway na kuvurunda kwenye fainal za kombe la Dunia.

Bao lao la kwanza lilipatikana katika dakika ya 58 ya kipindi cha pili wakati Welbeck alipomalizia shambulizi la haraka  lililohusisha nahodha wake Wayne Rooney na Raheen Sterling. 

Uingereza waliopeteza nafasi nyingi za kufunga walijihakikishia ushindi wakati Welbeck alipotia kambani bao lake la pili katika dakika za mwishoni kwenye dimba la St Jakob-Park. 






0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!