Na Oscar Oscar Jr
Kocha wa klabu ya Yanga Mbrazil Marcio Maximo ana mitihani mingi sana ndani ya klabu hiyo na ni lazima aweze kuifaulu ili kulinda imani na matumaini makubwa waliyonayo viongozi na mashabiki juu yake.
Kwa kuanzia Maximo atalazimika kuamua mchezaji wa kigeni wakubaki katika klabu hiyo kutokana na kuwa na wachezaji sita wa kigeni huku kanuni za ligi zikiruhusu wachezaji wasio zidi watano tu.
Emmanuel Okwi, Kiiza na Niyonzima ndiyo wachezaji ambao mmoja kati yao ni lazima atemwe na kwa taarifa ambazo sio rasmi, Hamisi Kiiza ndiye aliyekalia kuti kavu. Yanga ilimaliza msimu uliopita ikiwa timu yenye safu bora ya ushambuliaji kuliko yoyote ikiwa na mabao 61.
Mabao 12 kati ya hayo yalifungwa na Didier Kavumbagu ambaye ametimkia klabu ya Azam na 11 yakifungwa na Kiiza. Kama Yanga watamtema Kiiza, watakuwa wapunguza mabao 23 yaliyofungwa na wachezaji hao wawili kwa ujumla msimu uliopita.
Ligi yetu bado haizalishi mabao mengi sana kwa sababu, mechi nyingi msimu uliopita zilimalizika kwa sare ya bila kufungana na nyingi zilimalizika kwa kufungana bao 1-1.
Ukitazama timu zote 14 zilizoshiriki ligi kuu msimu uliopita utakutana na wachezaji saba tu ambao waliweza kufunga angalau mabao 10 na kati ya hao, Yanga inawachezaji watatu (Ngassa bao 13, Kiiza 12 na Kavumbagu 11)
Mara nyingi kumekuwa na malalamiko ya makocha kusajiliwa wachezaji wasiowataka lakini, Yanga wameweza kuliepuka hili na kumpatia jukumu Maximo mwenyewe.
Genlson Santos na Andrey Coutinho pengine walikuwa hawahitajiki pale Yanga lakini kutokana na kocha kupewa mamlaka wametuwa jangwani. Huu ni mtihani mwingine kwa Maxico kwa sababu kama wachezaji hao hawata fanya vizuri, gwaride linaweza kuja kumgeukia mwenyewe.
Mwisho kabisa, Yanga baada ya kuukosa ubingwa msimu uliopita kwa namna yoyote hawatoridhika na kumaliza tena kwenye nafasi ya pili au chini zaidi.
Ubingwa utamuweka Maximo huru katika kutenda kazi yake Jangwani. Hakuna anayejua namna timu mbili za wananchi zitakuja na ujio upi (Ndanda fc na Stand United) wakija kama Mbeya City itakuwa balaa. Vipi kuhusu uzoefu wa Polis Morogoro? muda uta amua.
Baada ya kuipata nafasi ya tatu na kupata mdhamini ambaye amewaongezea nguvu kiuchumi, Mbeya City nao watautaka ubingwa huku Azam wakitamani kuendeleza Ufame wa ligi kuu bara baada ya kuonja utamu wake msimu uliyopita.
Huwezi kuwasahau Simba ambao nao wanataka kurudisha heshima iliyopotoea kwa muda sasa, hii pia ni changamoto nyingine kwa Maximo.
Marcio Maximo ni kocha bora kutokana na falsafa zake na anazifahamu siasa za soka la Tanzania, muda utafika na kila kitu kitakuwa mezani.
3 August 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment