Na Abuu Hozza
0759422148
Mara ya mwisho kwa timu yetu ya taifa kushiriki michuano ya kombe la Afrika ni zaidi ya miongo mitatu iliyopita ambapo tulifuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika kule Nigeria.Zaidi ya hapo tumekuwa na historia iliyojaa kufeli na kushindwa kwenye mpira wetu.
TFF imekuwa ikiishi kwenye mipango mifupi ya voda fasta na kuacha kuwekeza katika mitazamo ambayo faida zake zinaweza kuwa za muda mrefu sana baadaye.
Mfano mpango wa kukusanya vipaji wa kutoka mikoani na wilayani wa hivi karibuni ambao umeshindwa kutoa matokeo yenye mwelekeo chanya.
TFF kama watawala wa mpira wa nchi hii ni ajabu kutowashutumu ama kuwapongeza kwa matokeo yeyote ya timu yetu. Hapana shaka kwamba mpira wetu umekosa uelekeo.
Kitu kikubwa kinachoumiza ni kwamba tunaleta siasa na kufanya mpira ni kama sekta ya kilimo ambayo tumeshindwa kuwa na mipango imara na endelevu ya kilimo cha kisasa na kubaki kutegemea wakulima wa jembe la mkono walishe taifa zima huku tukijidanganya kwamba nchi yetu inainuka kiuchumi.
Hivyo basi sasa ni wakati wa kuanza upya na kuachana na ubabaishaji uliotujaa vichwani mwetu na kuja na mfumo mpya kama taifa. Mfumo wa soka unaojali zaidi maslahi ya pesa kuliko hata mafanikio ya timu uwanjani hautatufikisha popote.
Ni aibu kubwa mno kwa nchi kubwa kama hii yenye wakazi karibia milioni 45 kukosa wachezaji imara wasiozidi 30 tu wakiwa wameandaliwa vizuri kiakili,kiufundi na kiushindani ili kuweza kushinda katika ngazi ya juu na kuleta sifa kwa nchi yetu, kwa hilo hatuna kisingizo cha kuepuka uzembe wetu.
TFF kama watawala wanajua kabisa mpira wetu haukui na uko taabani kimataifa hata mbele tu ya majirani zetu ambao kwa sasa wachezaji wao wengi wamejenga hulka ya kukimbilia hapa kwetu kwa ajili ya malisho bora yanayopatikana katika ligi yetu.
Lakini bado Shirikisho letu la soka limejisahu na kutoa macho zaidi kwenye Ligi Kuu ya vilabu ya Vodacom kuliko hata soka la nchi hii ambalo ndio msingi mkubwa wa uwepo wake.
Sehemu ya pili inafuatia hivi punde.....usikose!!!
0 comments:
Post a Comment