Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 August 2014
Friday, August 01, 2014

Je, wanayanga wako tayari?

 Na Oscar Oscar Jr


Kumekuwa na habari ambazo zimeenea kuwa klabu ya Yanga imejipanga kupeleka kikosi cha vijana na wachezji wake waakiba kwenye michuano ya Kagame ambayo inatarajia kuanza kutimua vumbi mapema mwezi huu kule Kigali-Rwanda. Bado benchi la ufundi la timu ya Yanga halijithibitisha madai haya ingawa tunaweza pia kuangalia faida kwa kutazama pambe zote mbili za vikosi.

Je, wana Yanga wako tayari?
Marcio Maximo ni kocha ambaye wanajangwani wanamatumaini makubwa sana juu yake na pengine kufanya vizuri kwenye michuano ya Kagame inaweza kuwa dalili nzuri kwao kuelekea kuanza kwa purukushani za ligi kuu. 

Yanga wametoka kupoteza ubingwa wao msimu uliopita mbele ya timu ya Azam kwa tofauti ya alama sita, Azam wakiwa na alama 62 huku Yanga wakiwa na 56 ni wazi kuwa kama watapata Ubingwa wa Kagame hali ya kujiamini itaongezeka kwa wachezaji na kwa sababu hii, sioni kama kuna maana ya kutotumia kikosi imara.

Idadi ya mashindano na mechi za ligi.
Ligi kuu Tanzania bara inahusisha michezo 26 pekee kutokana na idadi ya timu shiriki kuwa 14 hivyo Yanga atacheza mechi 13 tu kwenye mzunguko wa kwanza na 13 nyingine kwenye mzunguko wa pili. 

Mchezaji anakuwa fiti kucheza dakika 120 kila baada ya siku nne hivyo bado sioni kama Yanga wanahitaji kupumzisha wachezaji wao kwa kuhofia uchovu. Ukiachana na ligi kuu, Yanga watashiriki pia kombe la shirikisho barani Afrika na kwa ukubwa na uzoefu wa kikosi chao bado kikosi chao kina uwezo wa kumudu mapambano yote.

Kuwapa nafasi vijana.
Kama Yanga wataamua kupeleka kikosi cha vijana, ni wazi kuwa kutakuwa na faidi kwani vijana hao watapata uzoefu ambao utakuwa na tija siku za usoni. 

Maximo ni kocha anayependa sana kuwainua vijana kama alivyoonyesha wakati akiwa kocha wa timu ya taifa kwa kuwatumia kina Jerryson Tegete na wengine, bado anaweza kuwatumia kwenye michuano hiyo kina Amosi Adele, Khamisi Issa, Benson Mikaely kwa manufaa ya baadae.

Kuwapa nafasi wachezaji wa akiba
 Kutokana na ukubwa wa kikosi cha Yanga wachezaji wengi wa timu hiyo wamekuwa wakiambualia kukaa benchi na michuano hii inaweza kutumika kurejesha viwango vyao na imani kwa mashabiki. 

Ukitazama benchi la Yanga, unakutana na watu kama Said Bahanuz, Ally Mustapha na wengine kibao. Kama benchi la ufundi litawapa nafasi ya kucheza mechi za Kagame, itakuwa faida kwa wachezaji hao kwani wataitumia katika kujijenga na kumfanya kocha awaamini zaidi kueleka ligi kuu.

Bado uamuzi wa timu gani itakwenda kwenye michuano ya Kagame, unabaki mikononi mwa benchi la ufundi la Yanga linaloongozwa na wabrazil Marcio Maximo na Leonardo Neiva huku wakisaidiwa na wachezaji wa zamani wa timu hiyo Salvatory Edward na Shedrack Nsajigwa.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!