Searching...
Image and video hosting by TinyPic
2 August 2014
Saturday, August 02, 2014

Hata Mats Hummels hawezi kuisaidia Arsenal

Na Oscar Oscar Jr

Kuna taarifa za beki kisiki na nahodha wa timu ya Arsenal Thomas Vamerleen kutimka kwenye kwabu hiyo na kujiunga na ama Manchester United au klabu ya Barcelona. 

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger bado ni yule yule wa juzi jana na leo, hakubali mabadiliko. Bado ana amini katika muujiza wa soka kuliko uhalisia na si ajabu kocha huyu akawa ana amini kuwa kuna siku mshambuliaji wake Sanogo atafikia kiwango cha Thierry Henry!

Matatizo ya timu ya Arsenal msimu uliopita, hayawei kutatuliwa na usajili wa golikipa wala mabeki wawili wa kulia waliotuwa klabuni hapo. 

Ukitazama kikosi cha Arsenal hasa kwenye kiungo mkabaji, unagundua kabisa kuwa bado hakuna mtu wa kumuwekea dhamana. Unaweza kuwafunga Westham United lakini ikawa ngumu mbele ya Bayern Munich, unaweza kuona Flamini na Arteta waking'aa mechi dhidi ya Tottenham lakini ikawa ngumu mbele ya Chelsea na Manchester City.

Arsenal inahitaji watu wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi na Alex Song na Robin Van Persie, na sio ujio wa Calum Chambers na Methiew Debuchy ambao wanajaza nafasi za Bacary Sagna na Carl Jenkinson tu. 

Sina maana ya kupinga usajili wa mabeki hao lakini ninachokiona, ujio wa wachezaji hao ni kama "kubeep" tu na ndiyo maana, bado namsubiri mzee wenger apige.

Man United wanaposajili wachezaji kuziba nafasi zilizoachwa wazi na Patrice Evra, Nemanja Vidic na Rio Ferdnand  ni tofauti kabisa na Gunners. 

Moja kati ya matatizo yaliyowafanya United kutofanya vizuri msimu uliopita ni pamoja na walinzi hao kucheza chini ya kiwango.  wakati moja ya matatizo ya Gunners msimu uliopita, hayakuwa nafasi ya Golikipa wala mabeki wa kulia walionunuliwa klabuni hapo.

Mashabiki wa Arsenal wakisikia kuwa mzee Wenger anamuuza Thomas Vamerleen na kumnunua beki wa Borussia Dortmund Mats Hummels, wanaweza wakaanza kufanya sherehe kutokana na ubora wa mlinzi huyo wa Ujerumani na kusahau kuwa tatizo la msingi lililowanyima ubingwa msimu uliopita bado lipo pale pale.

Hongera sana Gunners kwa kumnasa "Mwanaume" Alexies Sanchez, hii ndiyo njia kuu ambayo mzee wenger anatakiwa kupita na kuachana na usajili wa michepuko ambao umekuwa hauna tija. Joe Campbell bado sio mchezaji wa kumtegemea kwa sababu bado ni mchanga na mgeni pia wa EPL ingawa ana uwezo mkubwa. 

Kama Wenger atamleta mtu wa aina ya Baloteli na kiungo wa aina ya Semi Khedira, Arsenal wanaweza kurudi kwenye ushindani na  Wakibakia kama walivyo, yanaweza kujirudia yale yale ya msimu uliopita.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!